Calisah Aanika Mastaa Aliobanjuka Nao

Mwanamitindo maarufu wa kiume Bongo ambaye pia hivi sasa ni Mr. Africa Calisah Abdul ameanika Listi nzima ya mastaa wa kike ambao amewahi kuwa nao kwenye mahusiano.

Calisah amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na Kipindi cha Ala Za Roho ya Clouds Fm ambapo alimsanua Diva The Bawse kuwa ameshakuwa kwenye mahusiano wasanii Kama Wema Sepetu, Irene Uwoya, na Jacqueline Wolper.

.

Calisah ameweka wazi kuwa alianza mahusiano ya kimapenzi na Wema wakati bado akiwa kwenye mahusiano na Idris Sultan bila Idris mwenyewe kujua.

Lakini pia Calisah ameweka wazi kuwa ameshawahi kuwa kwenye mahusiano na wasanii wa Bongo movie Kama vile Irene Uwoya na Staa mwingine Jacqueline Wolper.

Kwenye mahojiano hayo Calisah amekana  kuwa kwenye mahusiano na Hamisa Mobetto na Socialite maarufu kutoka Kenya Vera Sidika na kukiri iliyotrend kwenye mitandao ni Kiki.

Calisah Amwaga Povu Zito Baada Ya Kushinda Mr. Africa

Mwanamitindo wa kiume anayeendelea kufanya vizuri katika anga za kitaifa na kimataifa Calisah Abdulhamiid amefunguka na kutoa ya moyoni baada ya kutangazwa mshindi wa shindano la Mr.Africa.

BAADA ya kufanikiwa kushinda shindano la  Mr Africa International 2018, huko  nchini Nigeria, Calisah ameelezea furaha aliyonayo kwa sasa na kuwashukuru Watanzania wote waliompigia kura na kuilalamikia Serikali kutompa sapoti katika safari yake ya kuelekea nchini humo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Mara Baada ya kuibuka mshindi na kuiwakilisha vyema nchi yetu, Calisah alifunguka:

Kwa kweli nilifarijika sana baada ya kutangazwa kuwa mimi ndio mshindi, licha ya kwamba kabla ya safari yangu ya kuelekea Nigeria nilipitia changamoto nyingi ikiwemo kutopata ushirikiano kabisa toka kwa Serikali yangu, kwa sababu hata bendera niliyoitumia niliishona mwenyewe kwa fundi, hivyo nimepata tabu sana mpaka kufikia hapa”.

 

Calisah Aibuka Kidedea Mashindano Ya Mr. Africa

Mwanamitindo maarufu wa kiume Bongo Calisah ameibuka kidedea katika mashindano ya Mr. Africa yaliyojumisha nchi mbali mbali za Afrika na kufanikiwa kuwamwaga vijana wengine kadhaa.

Shindabo hilo lilifanyika mwishoni mwa Wiki iliyopita nchini Lagos, Nigeria na kushirikisha washiriki kutoka nchi mbali mbali za Afrika Kama vile Lesotho, Nigeria, Ghana, Cameroon na nyinginezo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Calisah ameshukuru Baada ya kupata ushindi wake na  kuandika:

Queen Vee na Calisah Wanasa Katika Penzi Zito.

Mwanamitindo mtanzania calisah anasemekana kunasa katika penzi zito na mwanadada kutoka uganda Queen vee ambae hivi karibuni alikuwa akilia kuteswa na mapenzi na mwanaume ambae alikuwa akimtumia kwa ajili ya jina lake na pia kutokana na pesa zake.

Wawili hao wanaoekana kuwa katika penzi jipya lakini pianwamekuwa wakishidwa kuficha mahaba hayo na kuitumia mitandao ya kijamii  kuanika mahusiano yao hadharani na mbele ya mashabiki.

Queen alikuwa na mahusiano na msanii Otile brown kwa muda mrefu kidogo lakini alikuja kulalamika hadharani kuwa mwanaume huyo amekuwa akimtumia kwa ajili ya mambo yake binafsi ya kujinufaisha kimuziki na kimaisha pia.

 

Nishatembea na Wanawake Zaidi ya Elfu Moja :-Calisah

MWANAMITINDO Maarufu  sana mjini kutokana na kazi yake, Calisah Abdulhamid amefunguka kwa mara nyingine tena na kusema  kuwa katika ukuaji wake mpaka sasa alipofikia sasa katika sanaa ameshatembea na wanawake wapatao elfu moja, kwa sababu ilifika kipindi kila siku alikuwa akitembea nao watatu

Calisah aliliambia Risasi Jumamosi kuwa, kabla hajawa staa alishatembea na wanawake kama wengi na baada ya kuwa staa akatembea na wengine zaidi na hii yote inatokea kwa sababu asilimia kubwa ya wanawake walikuwa wanajipeleka wenyewe.

Waache kujirahisisha na waamini kwamba wanaweza kuwatengeneza wanaume wao wenyewe, waache tamaa kuna watu wananitamani na wanataka kuwa na mimi kimapenzi kwa sababu nina jina, navutia, lakini hawajui kama kuna mtu alimtengeneza Calisah tangu yupo chini au kuna kipindi nakosa kabisa pesa, lakini kuna mtu ananielewa na maisha yanasonga mbele, hivyo nawasihi dada zangu wajiamini,” alisema Calisah

Waliyoiponda Nguo Yangu Wataiiga Hivi Karibuni- Calisah

Model na mwanamitindo maarufu Bongo, Calisah Abdulhamiid amefunguka na kudai kivazi alichovaa siku ya mashindano ya Miss Tanzania 2018 kitaigwa sana na watu hapo baadae.

Calisah alitengeneza headlines Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana na vazi hilo ambalo lilisemekana kuwa limekaa kwa kama blauzi ya kike kutokana na material yake na rangi.

Baada ya kipindi sana na watu kwa ajili ya kivazi hicho, Calisah amesema haoni tatizo la nguo ile na wanaomponda ndio watakuwa wa kwanza kuiga hapo baadae.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Calisah amesema kuwa sheria namba moja ya mitindo ni kuvaa chochote kile ili mradi kinamfanya mtu awe huru na mashabiki wasikariri kama kuwa mwanamitindo lazima uvae suti.

Ile nguo haina vifungo na kitu pekee kinachokufanya ujue nguo kama ni ya kike au ya kiume ni vifungo na zipu vinavyowekwa upande wa kushoto au kulia. “Ilikuwa na kamba kamba za silva na ni ya kiume kabisa. Najua wanaosema hivi utawaona wakiniiga hivi karibuni“.

 

Nilishawahi Kwenda kwa Mganga Lakini Sio kwa Sababu ya Demu:-Calisah

Mwanamitindo Calisah ambae mara nyingi amekuwa akisema ukweli juu ya maisha yake na maisha ya wasanii wengine amefuguka na kusema kuwa katika maisha yake aliwahi kwenda kwa mganga  lakini sio kwa sababu ya mwanamke ila kutokana na kujiweka imara yeye mwenyewe.

Calisah anasema kuwa hawezi kamwe kwenda kwa mganga ili tu kumloga mwanamke lakini kama ni mambo mengi  anaweza kwenda ingawa pia hawezi kwenda kwa ajili ya kumloga mtu yoyote kwa mafanikio ya kazi .

ndio nilishawahi kwenda kwa mganga lakini sio kwa sababu ya demu,haa siwezi kwenga kwa mganga kwa sababu i dont chase holes, nilikwenda kwa ajili ya mambo ya kimaisha tu lakini sio mapenzi.

Nilikwenda kwa mganga kwa sababu ya kujiweka vizuru tu mimi mwenyewe kwa sababu tunaishi na watu na kuna ma-haters pia lakini sijawahi kwenda kwa ajili ya kumloga mtu pia.

Ushaur wa Calisah kwa Mshindi Mpya wa Miss Tanzania.

Mwanamitindo Calisah alipata bahati ya kuongea na moja ya waandishi wa habari waliokuwa wakihoji watu mbalimbali katika ukumbi uliofanyikia mashindano ya Miss Tanzania mara baada ya mashindano kuisha ambapo mwanamitindo huyo alifunguka mambo maziti na kusemakuwa hasiige mkumbo wa ma-miss waliopita.

hasigawe sana chini,h asiwahi sana kugongwa ili kupata mafanikio kwa sababu kama kitu kipo kipo tu wala asiwe na haraka, kuna msanii aliwahi kusema kuwa wakujichunga ni wewe je umekosa cha kuuza mpaka ujiuze mwenyewe?, watumie vitu vyao vizuri ili waweze kufikia malengo yao wasivitumie ili kupata mafanikio kwa haraka .

Maneno ya calisah yanakuja kutokana na skendo nyingi sana zimekuwa zikiwapata ma-miss waliowahi kushinda huko miaka ya nyuma na kupata umaarufu ambao mwisho wake unashindwa kuwapatia heshima ya taji kubwa la kuwa Miss Tanzania kama waliowakabidhi wanavyokuwa wakilieshimu na kuwapatia.

Calisah Atangaza Kuja na Mikorogo Kwa Ajili Ya Wanawake

Mwanamitindo maarufu Kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa Calisah Abdulhamid amezidi kushangaza wengi baada ya kutangaza kuja na mikorogo kwa ajili ya Wanawake.

Calisah ameweka wazi kuwa ana mpango wa kufungua duka  lake ambalo atajikita katika kuuza vidonge ambavyo vitatumika kutakatisha ngozi za Wanawake.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Calisah ambaye amehusishwa mara kibao kubadili ngozi yake na kuwa mweupe, alisema weupe wake umetokana na AC za magari na si vinginevyo kama watu wanavyoeneza.

Hapana sijawahi badili rangi ya mwili wangu, mimi ndo nipo hivihivi tangu zamani, kubadili ngozi kwanza ni mambo ya kike ambayo sijawahi kufanya hivyo, hizi ni AC tu za magari halafu mimi ni mtu ambaye naamini sana kwenye muonekano wa kiume ndiyo mana hata nafanya mazoezi, kwa hiyo sijawahi kufanya hivyo kwa sababu hata familia yangu ni ya watu weupe.

Kwanza nipo mbioni kufungua duka la dawa za vidonge vya kung’arisha ngozi kwa wanawake ambapo Bongo hii hakuna, mimi ndiyo nimeagiza pekee na nitakuwa naziuza ofisini kwangu”.

Calisah amekuwa Kwenye headlines za Media mbali mbali tangu wiki iliyopita alipotangaza kufungua kampuni ya kuwapa Wanawake mimba.

Calisah Awaita Wachora Tatoo za Wapenzi WaoWashamba wa Mtwara.

Mwanamitindo Calisah  amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake hawezi kufanya ujinga wa kujichora tatoo ya jina la mwanamke aliyenae katika mahusiano eti ikiwa kamanjia mojawapo ya kumuonyesha kuwa anampenda sana.

Akiongea na moja ya waandishi, Calisah anasema kuwa kumekuwa na tabia ya watu kujichora tatoo za watu walionao katika mahusiano lakini kwa upande wake hiyo ni kama ushamba na amewaita watu hao washamba kama wamakonde kutoka mtwara.

Hii inaweza kuzua gumzo hasa kwa sababu amewataja kabisa na watu anaowafananisha nao lakini hayo ni maoni yake calisah.

Mwanamitido huyo hapa karibuni aliwahi kutangaza kuwa na kampuni inayohusika na kwa bebesha wanawake mimba .

Calisah Atangaza Kumiliki Kampuni ya Kuwapa Mimba Wanawake.

Mwanamitindo calisah amefunguka na kutangaz kuwa kwa sasa ana kampuni mbili kubwa ambazo ni ya kukuza vipaji vya  wanamitindo wachanga lakini pia kampuni kubwa nyingine aliyokuwa nayo ni ya kuwapa wanawake mimba ambao wamekosa mimba kwa wanaume wengine.

Mwanamitindo huyo anasema kuwa  mpaka sasa ameshafanikiwa kuwapa mimba wanawake kama 25  swala analofanya ni kumtafuta na kusainia nao mkataba na kulipana baada ya hapo mnaingia ndani na kukamilisha kazi yenu.

Mwanamitindo huyo alishawahi kufunguka na kusema kuwa wanawake weng wamekuwa wakimtumia meseji na kumtaka kimapenzi huku wengine wakitamani sana kuzaa nae kutokana na muonekano wake na ndio maana ameamua kuanzisha kampuni hiyo.

Calisah Kushiriki Mashindano Ya Mr. Africa 2018

Model na mwanamitindo maarufu Bongo anayejuliakana kama Calisah amefunguka na kueleza Bahati ya mtende iliyomuangukia ya kwenda kushiriki mashindano ya Mr. Africa mwaka 2018.

Calisah amedondokewa na zali la kwenda nchini Nigeria kwa ajili ya kushiriki Shindano la Mr Africa International, ambalo linachukua mtu mmoja toka Afrika na kumpeleka nchini humo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Calisah amesema kwamba imekuwa ni furaha kubwa sana kwake kualikwa kwenda nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mr Afrika, hivyo anaimani kubwa kuwa atafanya vizuri na Tanzania itakuwa namba moja na ndiyo maana sasa hivi anafanya sana mazoezi.

Nilitumiwa barua mwaka jana ya kwenda kushiriki Mr Africa International, lakini nilishindwa kwenda kwa sababu kwanza nilichelewa kupata barua yao halafu pia nilitakiwa kujilipia tiketi ya ndege mwenyewe kwenda na kujilipia hoteli kwa siku kadhaa ambazo ningekuwepo huko.

Lakini kwa bahati nzuri tena mwaka huu wamenitumia tena mwaliko, kwa hiyo natakiwa kwenda Nigeria mwezi wa 10 kwa ajili ya hayo mashindano na mimi ndiyo Mtanzania pekee ambaye nimechaguliwa kwenda na ninajua kabisa nitashinda”.

 

Calisah Aongea Mazito Kuhusu Kuwapa Ujauzito Wadada wa Mjini.

Kijana anaesifika kwa kazi yake nzuri ya modelling, Calisah amaefunguka na kusema kuwa amekuwa akiwapa mimba wadada wengi wa mjini mabao wamekuwa wakimuomba kufanya hivyo karibia kila siku.

Akiongea na mtangazaji wa Dizzim online , Calisah anasema kuwa wadada wengi wamekuwa wakimsumbua sana kufanya nao mapenzi ili wapate mimba yake na yeye hana kinyongo na hilo kabisa kwa kuwa anaamua kuwasaidia kama binadamu.

nimewatoa wadada wengi sana mimba na wengine wamekuwa wakinimba niwape, wako wanawake wengi sana  ambao wamekuwa wakiomba niwape mimba wanakaribia hat 25, hata nikikuomyeshea kwenye simu yang wapo wapo.(huku akifungua simu yake), na pia huwa naangalia mi mwenyewe kwa sababu hata mimi nina tamaa vilevile kwaio naangalia kama mzuri napita na wewe kama mbaya naachana na wewe.sina uwezo wa kuwalea wote hao  ila hata mimi niko kwenye mchakato so soon ntapata mtoto.

Pretty Kind na Calisah Wadaiwa Kuwa Kwenye Penzi Zito

Muigizaji wa Bongo movie na msanii wa Bongo fleva Suzan Michael amedaiwa kuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na Model maarufu Calisah Abdulhameed.

Calisah ambaye ameshakuwa Kwenye Mahusiano na mastaa kadhaa kama vile Jacqueline Wolper na Wema Sepetu amesemekana kuweka kambi kwa Pretty Kind.

Global Publishers wanaripoti kuwa chanzo ma­kini kilieleza kuwa Pretty Kind amekuwa akioneka­na mara kwa mara maeneo ya Sinza, Dar akiwa na Calisah wakionyeshana mahaba niue hivyo ndiye mtu wake kwa sasa.

Baada ya Tetesi hizo kusambaa hivi karibuni gazeti hilo lilimsaka Pretty Kind ili kujua ukweli wa mambo Lakini mara moja alikataa taarifa hizo na kudai Hazina ukweli wowote.

Siyo kweli tupo karibu na Calisah kwa sababu ya kazi na siku ikimalizika mashabiki wataiona”.

 

Calisah Amefunguka Kuhusu Mkwanja Mrefu Aliopata Baada ya Kuvaa Viatu Vya Kike

Mwanamitindo maarufu anayejulikana kama Calisah amefunguka na kudai kuwa kwa mwaka huu wa 2017 hakuna kazi iliyomuingizia kipato kikubwa kama kuvaa viatu vya kike.

Mwishoni mwa mwaka huu Calisah alizua gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kurusha picha kwenye Instagram akiwa amevaa viatu vya kike jambo lililo washangaza watu wengi huku kila mmoja akitafsiri kitendo kile kivyake lakini mwenyewe alijitetea na kudai kuwa ilikuwa ni kazi to Kama kazi nyingine.

Kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa redio kupitia kipindi Chao cha Planet Bongo Calisah amefunguka na kudai kuwa dili hilo alilipata kwa ajili ya kutangaza viatu vya kike Instagram kutoka kampuni Fulani na dili hilo lilimuingizia kiasi cha shilingi milioni saba za kitanzania.

Hili lilikuwa ni moja kati ya dili lililoniingizia hela ndefu kwa mwaka 2017 hadi mpaka hivi sasa ninavyoongea bado limevunja rekodi sijawahi kupata dili kama lile hata matangazo niliokuwa nayafanya tofauti tofauti kwa kipindi kile hayajafikia ile amount niliyolipwa kwa kuvaa vile viatu vya kike”.

Baada ya picha hizo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kila mtu aliongea lake na hata wapo waliodai kuwa Calisah atakuwa ni shoga kutokana na kuvaa viatu vya kike jambo alilokataa kwa nguvu zote na kusisitiza kuwa yeye ni rijali na wala sio shoga.

Daxx Cruz Asema Kitendo Alichokifanya Calisah Ni Aibu

Mwanamitindo wa kimataifa anaefanya vizuri katika kazi zake kutoka Tanzania ambae anaishi  na kufanya kazi zake Afrika ya Kusini, Daxx Cruz amefunguka na kuongelea kitendo alichokifanya mwanamitindo mwenzake anaechipukia calisah na kusema kuwa ni cha aibu hata kama analipwa ela. mwanamitindo huyo amedai kuwa kitendo icho cha yeye kufanya kazi za kike ni kuiaibisha tasnia hiyo.

Calisah ambae wiki chache zilizopita alionekana kupata donge nono la kufanya kazi ya kupiga picha akifanya marangazo ya viatu vya kike ilhali yeye ni mwanaume , hata hivyo baada ya kuzagaa kwa picha hizo katika mtandao baadhi ya watu walianza kumsema na kukashifu kitendo icho kuwa ni tabia mbaya .
hata hivyo calisah mwenyewe hakuonekana kujali baadhi ya maneno ya watu katika mitandao badala yake alisema kuwa yeye ana uwezo wa kufanya kazi zote ilimradi tu kazi iyo iweze kumlipa ela itakayo msaidia kumudu maisha yake.

Akizungumza kwenye bongo magazine, Daxx Cruz anasema kuwa hata yeye yupo katika tasnia hiyo ya modelling kwa muda mrefu lakini hawezi kufikia hatua ya kufanya kazi kama hizo kwa sababu ni kazi ya kike na wapo models wa kike na kwa mwanaume aliekamilika hawezi kufanya kitendo kama hicho ambacho hajawahi kuona kimetokea  Afrika.Kwa kuongezea Daxx Cruz amesema kuwa kitendo alichokifanya Calisah ni kitendo cha aibu

Daxx Cruz ni mmoja wa wanamitindo wanaofanya vizuri nje ya tanzania, akiwakilisha tanzania na ameweza kuitangaza vizuri tanzania.hata huivyo sio mara ya kwanza kwa Daxx Cruz kumuongelea Calisah, mara ya kwanza alishawahi kusikika akisemakuwa Calisah hafai kuwa model kabisa na wala hana sifa za kufanya kazi hiyo, endapo ataenda nje ya Tanzania hatopata soko la kufanya modelling kabisa.