Tamasha maarufu nchini Tigo Fiesta la mwaka 2018 linatarajiwa kufanyika rasmi jijini Dar Wiki ijayo ya Tarehe 22 katika viwanja vya Posta.
Fiesta tayari ilifanyika karibia mikoa 15 nchini Tanzania lakini ilipofika wakati wa kufanyika hapa Dar Es Salaam ambayo ndio ilikuwa inafunga msimu mpya wa Fiesta ilisitishwa kwa madai kwamba sehemu ambako ingeenda kufanyika ingeleta taharuki kutokana na kelele zitakazojitokeza mahala hapo.
Uongozi wa Clouds Media Group Kupitia ukurasa wao wa Instagram umetoa taarifa hii kuhusiana na tamasha hilo:
Tarehe 22 Desemba kwenye Viwanja vya Posta jijini Dar es Salaam, Machampion wote wa nchi wanakwenda kutoa shukrani moja kubwa na kushangalia mafanikio ya mwaka huu. Ni mara 2 ya tulichokimiss: stage ya viwango, sound kubwa kuliko, bata la kihistoria na list ndefu ya machampion. . #TigoFiesta2018, ”