‘Sasa Mimi Ni Mtu Mpya’ Amekiri Dudubaya Baada ya Kudai Kamrudia Mungu

Msanii mkongwe wa Bongo fleva maarufu kama Dudu Baya amefunguka na kuielezea hadhara katika barua ya wazi kwamba ameamua kumrudia Mungu.

Dudu Baya alishika sana vichwa vya habari kwa mwaka uliopita wa mwaka 2017 kuanzia bifu lake na msanii mwenzake Mr. Nice kunyemelea kutaka kirudi tena na wawili hao kusikika wakianza kurushiana tena maneno upya mpaka ishu ya Young Dee kuiba wimbo wake.

Lakini Dudu Baya amesema anauanza mwaka huu wa 2018 upya kabisa huku akidai kwamba ameamua kumrudia Mungu wake na kuachana kufanya matendo ambayo hayampendezi.

Dudu Baya amefunguka hayo kwenye mahojiano na Bongo 5 ambapo amedai kuwa hii ni barua ya wazi na shukrani yake kwa kuuona mwaka 2018:

Eeh Mwenyezi Mungu Muumba wa mbingu na nchi na mimi mwanadamu na vitu vyote vilivyomo asante baba mwezi wa tano mwaka 2017 nilimchoka shetani wa pombe si rahisi kumuacha kama mtu hajakushirikisha wewe mwenyezi Mungu huwezi kumuokoa asiye tayari kuokolewa 2017 asante baba umeniokoa mwaka 2018 nauanza nikiwa mamba Dudubaya, oil chafu konkii master new person new life pombe alininyima muda wa ibada pombe alininyima muda wakutimiza majukumu yangu pombe alininyima muda wa kuzuia hasira zangu sasa mimi ni mtu mpya”.

T.I.D Awaachie Hayo Mambo Gigy Money Na Amber Lulu -Dudubaya

Wiki iliyopita kuna picha zilikuwa zimetanda sana katika mtandao wa kijamii wa instagram ukimuonyesha msanii T,I,D akiwa kitandani na mwanamke huko wakionekana kuwa faragha, mashabiki wake walikuwa wakiiuliza kuhusu picha hizo zimetokea wapi, je kuna video mpya inakuja au vipi.

Msanii mkongwe wa bongo fleva Dudubaya ameamua kuongelea swala hilo akiwa kama mtu wa karibu wa T.I.D lakin pia kama msanii mwenzie mkongwe walioanza muziki kipindi cha nyuma kidogo,akiongelea picha hizo Dudubaya anasema kuwa kwa umri na heshima aliyonayo T.I.D  hakupaswa kufanya mambo kama hayo kwa sababu kwanza anae mtoto mkubwa  ambae endapo atakuwa ameona picha hizo itakuwa imeleta pichambaya , lakini pia akiwa kama msanii mkongwe mambo ya kutafuta kiki kwa kupiga picha za hivyo anapaswa kuwaachia kina Gigy Money na Amber Lulu, hayo mambo yeye hayamfai tena.

“Picha ya T.I.D  nimeiona  kimaadili sio picha nzuri kwa age yake yeye maana tayari anamtoto, Tid juniour, mimi ninamjua ni mkubwa na anajitambua kabisa, lakini pia sisi ni kizazi cha analogi, na sasa hivi ni kizazi cha digitali na kizazi cha digitali kikikuteka basi usiwe kama Amber Lulu au Gigy Money, ambao ni kizazi cha digitali, waachwe wafanye mambo yao ya kidigitali,” aliongea dudubaya

Dudubabya anaongeza na kusema kuwa ingawa kwa sasa ni lazima ufanye kitu kikupe kiki lakini hayo hayafai kwa T.ID”wasanii wengi underground wanakwambia ili uweze kujulikana lazima ufanye kitu upate kiki,..lakini unapotengeneza kiki ni lazima uiangalie je iyo kiki unayoitengeneza yupo nani nyuma yako, mama yako, babako , kuna watoto wako.’  aliongeza Dudubaya.

Inawezekana ndivyo wasanii wengi wanavyoamini kuwa katika kufanya muziki ili watu wakujue na upate jina basi ni lazima ufanye jambo la aibu ili uweze ku-trend katika mitandao, lakini kumbe sio kwa sababu unapaswa kwanza kuangalia heshima yako lakini pia kile unachokifanya kina athari gani kubwa zaidi ya kile unachokitafuta kwa muda huo.Wasanii wanapaswa kujifunza kitu kutokana na hilo.

 

Picha ya T.I.D iliyosambaa kwa kasi katika mtandao hasa wa instagram.

 

Dudu Baya amsifia Chidi Benz

Msanii mkongwe katika  style ya ku-rap nchini Tanzania  tangu miaka ya 90’s mpaka sasa  na msanii ambaye ukitaja  wasanii wakubwa wakongwe  waliosaidia kukuza na kuinua muziki wa Tanzania basi huwezi kumuacha msanii huyu, si mwingine ni Dudu baya,Dudu baya ni msanii wa Bongo Fleva  ambae amepitia mengi  mpaka kufikia hapa alipo katika muziki.

Akiongea katika interview aliyoifanya hivi karibuni kupitia kipindi cha eNews cha EATV Dudu baya ameonekana kumsifia msanii mwenzie ambae pia ni mkongwe katika fani hii ya muziki Chid Benz,pamoja na kwamba katika kumbukumbu inaonyesha kuwa Dudu baya ni moja kati ya wasanii ambao waliongea vibaya kuhusu maisha ya msanii Chid Benz hapo awali na kumponda huku wakisema kuwa hawezi kubadilika tabia yake ya kutumia madawa ya kulevya na wala hatoweza kusikiliza watu wanachomwambia. lakini leo ameamua kubadilika na kumsifia Chid Benz, na anaamini kuwa Chid amebadilika .

“Nampa big up, amerecover ,namsifia sana ,sina doubt na yeye na namkubali sana “,  pia alimpa ushauri Chid “ni kama mdogo wangu, mimi ni kaka yake, sitaki arudi tena kwenye madawa ya kulevya,Mungu amuinue,Mungu amsamehe,na Roho Mtakatifu amsaidie  “aliongeza Dudu baya huku akimuombea pia.

Alipoulizwa kwanini mara ya kwanza alikuwa akimponda na sasa hivi anaonekena kumsifia ,Dudu baya alijibu” baada ya kuona anaelekea ninapopata…na tulishakutana mara mbili namuona yuko fresh.. kwenye mic namkubali, ana pumzi…hakuna Dar Es Salaam bila KingKong’ aliongezea Dudu baya.

Hata hivyo Dudu baya alisema kuwa “Mungu alisema tuombeane, mimi ninamuombea,shetani yule aliyemkamata kipindi kile asimrudie tena”

Chid Benz pia ni msanii mkongwe wa Bongo Fleva ambae alikumbwa na kashfa ya utumiaji wa madawa ya kulevya, ambapo matumizi hayo yalimpelekea kushuka kimuziki na kupotea katika ramani ya sanaa, lakini kwa sasa Chid amerudi tena huku bado akisuasua kidogo, hivyo Dudu Baya kama msanii mkongwe pia aliamua kumuongelea msanii mwenzie na kumpa moyo ili aendelee kufanya vizuri katika kazi zake.