Ebitoke Amefungukia Tuhuma za Kuiba Mume wa Mama Ashura

Mchekeshaji maarufu kutoka Timamu Tv Ebitoke amefungukia tuhuma ambazo zimekuwa zikimuandama kwa muda sasa kuwa yeye na mchekeshaji mwenzake Mama Ashura wana bifu baada ya kumuibia mume.

Ebitoke  alijipatia umaarufu siku za nyuma Kutokana na vituko vyake na make up yake ya sioni ameongelea habari ambazo zinaongelewa sana mtandaoni kuwa ameiba mume wa Mama Ashura ambaye amezaa naye.

Miezi michache iliyopita Mange Kimambi alivunja bonge la habari iliyowashangaza watu wengi kuwa Ebitoke anamchukua mume wa Mama Ashura ambaye pia ni Bosi wao anayewasimamia kazi zao pale Timamu Tv.

Pia ilisemekana kuwa tangu Ebitoke amchukue mume wa Mama Ashura wamekuwa kwenye bifu kali na pia ilisemekana kuwa Mama Ashura amekuwa akiteswa sana na mwanaume huyo.

Tangu taarifa hizi zienee Mama Ashura amekuwa haonekani Tena kwenye mitandao ya kijamii kama zamani na kuna hata taarifa kuwa hivi sasa mrefu kuzaa hapo Timamu Tv.

Ebitoke alifanya Interview na Millard Ayo Tv ambazo alipoulizwa kuhusu ishu yake ya Kumuona mume wa Mama Ashura alikataa kata kata kujibu tuhuma hizo:

Bwana hayo mambo mi sitaki kuyaongelea yaani ukiniuliza kuhusu huyo mtu sina cha kujibu lakini yupo tu mbona sema sitaki kumuongelea kabisa”.

Hata Ebitoke alivyobanwa na ndugu mtangazaji aeleze Mama Ashura alipo alikata kuendelea kufanya Interview na kuondoka.