Fid q,aongea na kina dada.

Msanii maarufu wa Hip-Hop  kutoka jijini Mwanza Farid Kubanda,

ameelezea jinsi anavyoshangazwa na tabia za kinadada wanapojiandaa kupata mimba kutoka kwa wapenzi wao bila hata ya kuwashirikisha wenzi wao katika swala ilo,Fid Q anasema kuwa ili kupata mtoto ni lazima kuwepo na makubaliano baina ya watu wawili.Akiongea katika kipindi cha eNewz kutoka televisheni ya EATV Fid Q anasema kuwa  “ongea na mtu mkubaliane  na siyo unajitegesha kwa mwenzio ili upate mtoto.Maisha siku hizi magumu sana,watu wanaishi kwa mipango na ratiba ya mwaka”.

 

Hata hivyo,mwandishi huyo  alipomuuliza msanii huyo  kuhusu swala la kuoa,

Fid q alisema kuwa kwa upande wake bado sana kuoa , anasema kuwa katika vitu vya kukosea basi kuoa upaswi kukosea hivyo bado yupo anatafuta yula ambae atakuwa na zile sifa ambazo yeye anafikiria ni lazima mke wake wa kumuoa anapaswa kuwa nazo.Fid q anasema swala la kuoa ni swala nyeti sio la kukurupuka,”ukikosea mke wa kuoa unaweza kuharibu maisha yako yote”