Mchekeshaji Steve Nyerere awekwa motoni kutokana na sakata ya kimapenzi ya Wema Sepetu na Freeman Mbowe

Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA, Freeman Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai na Wema Sepetu wamekua wakitawala vichwa vya habari tangu sauti (voice note) ambazo zinadaiwa kuwa zao kuenea kwenye mitendao ya kijamii.

Voice note hio inaashiria kuwa Freeman na Wema Sepetu wana uhusiano wa kimapenzi lakini wawili hao walikana dhana hii.

Mchekeshaji Steve Nyerere amejipata pabaya kuhusu sakata ya Wema Sepetu na Freeman Mbowe. Mashabiki wa Wema na Freeman wanadai kuwa sauti ya kiume iliyoskika kwenye voice note hio ya utata ni ya Steve Nyerere.

Steve Nyerere na Wema Sepetu

Nyerere ako na kipaji cha kuigiza sauti mbalimbali za viongozi wa kisiasa na watu wengine mashuhuri; na  hii ndo sababu ya watu kumlimbikizia lawama.

“Sio mimi yule na siwezi kufanya kitu kama kile. Ile sauti ukiisikiliza kwa makini utajua sio mimi na siwezi kufanya hivyo,” Steve Nyerere alijitetea kwenye mahojiano na Bongo 5.

 

 

Ukweli wadhihirika kuhusu uhusiano wa Wema Sepetu na Freeman Mbowe

Siku chache zilizopita voice note ambayo inadaiwa kuwa sauti ya Wema Sepetu and mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelao CHADEMA ilisambaa kwenye mtendao wa kijamii.

Wema Sepetu na Freeman Mbowe

 

Mazungumzo kwenye voice note hio unadhihirisha kuwa Freeman Mbowe na Wema Sepetu wako na uhusiano wa kimapenzi.

Mbowe hata hivyo amefunguka na kueleza ukweli wa maneno kufwatia kuibuka kwa voice note hio; mwenyekiti huyo wa CHADEMA alikana kuwa sauti iliyoskika kwenye voice note hio ni yake.

https://www.youtube.com/watch?v=0iZg-JoIRgc

Alisema kuwa hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Wema Sepetu. Mbowe alieleza kuwa maadui wake wanamchafulia jina kwasababu Wema Sepetu alijiunga na CHADEMA.

Skiliza maelezo ya Mbowe kwenye video hapo chini:

https://www.youtube.com/watch?v=Vfxtv8s08io