Gadner Afungukia Tetesi Za Kurudiana na Lady Jay D

Mtangazaji wa Clouds Fm Gadner G Habash amefungukia tetesi zilizosambaa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa amerudiana na aliyekuwa mke wake  Lady Jay Dee.

Siku chache zilizopita Gadner aliposti picha ya kitambo kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na mwanamuziki huyo nchini Kenya kwenye sherehe za utoaji wa Tuzo za Kisima. Katika tuzo hizo za miaka hiyo, Jide alitwaa Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike wa Afrika Mashariki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Gardner alisema kuwa anashangaa kwa nini watu waliona ni kitu cha ajabu kwa sababu ni ukweli ulio wazi kwamba hajawahi kuacha kumkumbuka wala hajawahi kumsahau mtalaka wake huyo.

Labda niseme wazi kwamba mimi sijawahi sijawahi kumsahau Lady Jaydee, ndiyo maana mtu akiniambia nimemkumbuka, nashangaa kwa sababu mtu unayemkumbuka ni yule uliyemsahau. Lakini kwangu yeye (Jide) sijamsahau hata kidogo, yupo tu siku zote kwenye akili yangu”.

Gadner alipoulizwa kama kuposti picha huko kunaashiria dalili za kurudiana na kurejesha ndoa yao upya, Gardner alicheka mno na kusema alifurahishwa na jambo hilo, lakini kwa sasa angeomba liachwe hivyohivyo.

Hilo la kurudiana? Kwa kweli naomba tuliache kwanza, tuliache hivyohivyo tu”.

Gardner na Jide walifunga ndoa Mei 14, 2005, lakini hawakubarikiwa kupata mtoto. Baada ya mvutano wa muda mrefu, wawili hao walifikia hatua ya kufikishana katika Mahakama ya Mwanzo ya Manzese jijini Dar na mahakama kuamua kuvunja rasmi ndoa yao ya Kikristo na kila mmoja kupewa hati yake ya talaka Agosti, 2014.

Gadner Alizwa na Pengo la Ruge Mutahaba Fiesta

Kwa muda sasa tangu tamasha la tigo fiesta limeanza na mpaka sasa linakaribia kumalizika , kumekuwa na pengo kubwa sana kwa tamasha hilo na kila kitu kinachoendelea ambacho kilizoewa kufanywa kwa utaratibu mzuri pengine hasa katika ufahamu mzuri zaidi kutokana na ukweli kuwa Bosi Ruge Mutahaba alikuwa ana mchango mkubwa sana katika tamasha hilo.

Ruge alikuwa akizunguka na wasanii katika kila mikoa kuhakikisha kuwa wasanii wamekuwa katika wakati mzuri wa kufurahia tamasha lakini pia kuhakikisha mashabiki pia , lakini pia alikuwa mtu wa kujitoa sana katika jamii ukiachilia mbali mawazo yake yaliyokuwa yenye thamani kila semina ya kila mkoa aliyokuwa akienda.

Kama utakumbuka kuwa tangu mwezi june bosi huyu amekuwahaonekani katika media na kazini pia kama wanavyosema wafanyakazi wake, swala ambalo liliwaumiza wengi kutokana na kwamba ugonjwa uliomshika alihitaji muda mrefu wa mapumziko kuliko kazi.

Gadner g Habash anaelezea swala la kutokuwepo kwa Ruge jinsi lilivyoweka pengo kubwa sana katika msimu huu wa fiesta kwa sababu ukweli uatabaki uwa alikuwa mtu mwenye mchango mkubwa sana kwa tamsha, kwa wasanii na hata mashabiki zake pa.

Sikutaka Kuwa Meneja wa Karen, Nilitaka Asimame Mwenyewe;-Gadner

Baba mzazi wa mwanadada Karen (GADNER)  amefunguka na kutoa sababu kwanini amekuwa hajihusishi sana na mswala ya muziki ya mtoto wake ikiwa hata yeye yuko katika maswala ya burudani kwa muda mrefu na ukizingatia kuwa amekuwa na jina kwa muda mrefu hivyo ingeweza kumfanya mtoto wake kuwa maarufu na kukuza jina kwa haraka.

Gadner anasema kuwa hakutaka kumsimamia karen kwa sababu alitaka mtoto wake asimame kwa miguu yake na kujivunia mahangaiko yake na sio kuwa nae kila muda, lakini pia Gadner anasema alitaka karen ajitangaze mwenyewe na wala sio kwa kutumia jina lake yeye .

mara ya kwanza nilishauriana na Ruge Mutahaba  kuhusu karen kwa sababu sikutaka kuwa meneja wake na nilitaka asimame mwenyewe, nilitaka ajitambulishe mwenyewe kwa mashabiki zake na  bila kutumia jina langu  ila ikitokea amelta ngoma yake kwenye radio nitamsapoti lakini kwa sasa anafanya kazi yuko chini ya uongozi unaomsimamia.;- Ameongea Gadnr alipokuwa katika mahojiano ya asubui na Clouds360.

Karen ambae kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa lawama na ule uliotoka hivi karibuni wa washa ni mtoto wa kike wa pekee wa mtangazaji Gadner Habash , mtangazaji maarufu kutoka Clouds media.