Aunty Ezekiel ataja njia aliyotumia kupunguza unene wa mwili wake!

Mrembo wa filamu Bongo za bongo Aunty Ezekiel amefunguka kueleza namna alivyoweza kupunguza mwili wake ulionenepa baada ya kuzaa cookie miaka 3 iliyopita.

Aunty Ezekiel

Muigizaji huyu alisema kuwa alishindwa kupunguza mwili wake hata baada ya kujaribu njia kadhaa. Akizungumza na motomoto news mrembo huyu alisema kuwa ilimbidi kusafiri hadi nchini Thailand kufuata dawa ya kupunguza unene.

Hii ni baada ya kuona kuwa mwili wake ulikuwa unanenepa na kwa sababu ulimnyima raha na kumfanya aonekane mzee basi akaenda Thailand ambapo alipata dawa inayomsaidia sana. Ezekiel alisema;

“Dah, yaani hata nikivaa nguo najiona wazi sipendezi hivyo katika pitapita yangu nikaambiwa kuna dawa nzuri Thailand, nikaenda na baada ya kuanza kutumia, naona ina manufaa makubwa na nadhani inaweza kuwasaidia watu wengine wasiopenda unene,”