Kajala atokwa na machozi baada ya haya kumtokea jijini Mwanza

Muigizaji wa filamu Kajala aliachwa na maumivu mkononi baada ya kunyofolewa kucha na mashabiki waliokuwa wakimvuta akiwa jijini la Mwanza.

Kajala Masanja

Akiongea na Risasi Jumamosi, Kajala alisema kuwa haya yalitokea akiwa kwa harakati za kufanya kazi anayoifanya na kampuni ya mchezo wa kubahatisha.

Kajala alisimulia kusema kuwa kucha yake ilitolewa akigawa tisheti kwa mashabiki ambao walianza mvutano na kwa bahati mbaya, kumvuta mkono mpaka kumbandua kucha aliyokuwa amebandika.

Jeraha hili lilimuacha huku akivuja damu mkononi na kuhisi uchungu ambao ulimfanya kulia. Kajala alisema,

“Yaani mimi nilikuwa sina ili wala lile nagawa matisheti mara wakaanza kunivuta kwa nguvu mpaka wakaitoa kucha yangu, hali hiyo ilinitesa asikwambie mtu jeraha la kucha linauma sana. Maumivu niliyopata yalikuwa ni makali mno kiasi ambacho nilishindwa kufanya kazi yangu, nilipata matibabu ambapo kwa sasa naendelea vizuri,”