Tazama picha mpya za Elizabeth Micheal ‘Lulu’ zinazo wazingua mashabiki

Muigizaji wa filamu Elizabeth Micheal ni mmoja wa mastaa wa kike kutoka bongo wanaowazingua mashabiki kutoka Afrika Mashabiki.

Hivi karibuni Lulu aliachia picha mpya akionekana amependeza na nguo ndefu kama ya mama yake aliyepigwa picha na true na mdogo wake wa kiume.

Sio siri kuwa Lulu ni mwanamke anayejitambua na mwenye ameumbika kama malaika. Ni wengi ambao wanazinguliwa na uzuri wake na pia roho yake safi.

Tazama picha hizi alizoziachia hivi karibuni huku akionekana na familia yake.

Lulu Amber na Jaguar kutoka Kenya kuachia wimbo pamoja?

Lulu Amber ambaye ni msanii mkubwa sasa kutoka Tanzania hivi karibuni alisema kuwa anamkataba na msanii kutoka nchini Kenya,Jaguar.

Amber Lulu

Muimbaji huyu alifunguka kudai kuwa Jaguar atakuwa anasimamia kazi zake wakati wowote anataka kuingia kwenye soko la Kenya.

Akizungumza na Showbiz xtra, ,Lulu alisema hili jambo la kujivunia kupata msanii kama jaguar kumpa shavu. Lulu aliendelea kusema kuwa hakuwa anatarajia jambo kama hilo kufanyika lakini anashukuru. Lulu alisema,

“Namshukuru Mungu kwa hili, nimepata mkataba mnono kwa Jaguar, makazi yangu yataendelea kuwa Bongo, lakini inapotokea nikahitajika Kenya nitakuwa nafika kwa wakati, niwaombe mashabiki wangu waendelee kunisapoti, naamini nitafika mbali zaidi na kuiwakilisha vyema nchi yangu,”

Hata hivyo bado anaendelea kufanya kazi zake za bongo.