“Nawasihi wakongwe ambao hawajaoa nao waoe kwani” Profesa Jay asema!

Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule anayefahamika sana kama Profesa Jay amefunguka kuwasihi wakongwe wa muziki kutia bidii ili pia wao waweze kuoa kama alivyofanya hivi karibuni na mpenzi wake, Grace.

Profesa Jay

Profesa Jay ambaye alianza muziki akiwa na umri mdogo ameonelea kuwa wasanii ambao wamekuwa naye kwenye muziki kwa miaka mingi pia waoe kwani Mungu atawapa baraka zaidi, baada ya kutulia na mwanamke mmoja badala ya kuwabadilisha kila wakati,

Rapa huyu wa bongo alisema haya akizungumza na Wikienda huku akisema,

 Nawasihi wakongwe ambao hawajaoa nao waoe kwani pale wanapokabidhi mapenzi yao mbele za Mungu ndipo baraka zaidi na neema za Mungu zinaambatana nao katika maisha yao yote kwa sababu ndoa ni furaha na amani pia.

Hata hivyo AY ameonekana kuzifuata nyayo zake baada ya kumvisha (engage) Pete mrembo wake siku kadhaa zilizopita.