Mama Diamond Azidi Kumpigilia Msumari Wa Moto Hamisa.

Mwaka unaenda kuwa mwisho na mambo yanazidi kupamba moto katika mitandao ya kijamii hasa baada iya familia hzi mbili ya Diamond Platinumz na ya Hamisa Mobeto kuwa katika vita isiyoisha ambayo ilikuwa imelala kwa kipindi fulani lakini sasa inakuja tena kuwa mpya hata zaidi ya mwanzo na  kwa kasi, na hii inaweza kuwa  itakuwa ni vita kubwa ya watu ,maarufu  ya kufunga mwaka .

Vita hii ilianza tena upya ambapo kwamuda ilikuwa kimya , hii ni  baada ya Hamisa na Zari kujikuta tena katika sehemu moja wakiwa kama wanatengeneza ushindani wa kujaza watu katika party mbili tofauti katika nchi moja nchini Uganda, vita ambayo imekuwa mpya tena hasa baada ya wanawake hao kujikuta wakioneana wivu kutokana na kuzaa na bwana mmoja na kila mtu akionekana kutaka ku-creat attentionkwa mashabiki kuwa bwana yupo upande wake.

Vita hii sasa imewaingiza mpaka watu wa karibu wa familia ya Diamond na Hamisa hasa   mama zao kwa pande zote mbili,hivi juzi mama mzazi wa Diamond ametupa dongo lingine kwa kumwambia kuwa kama yeye ni mbu basi haina haja ya kupigwa bunduki bali dawa yake ni Expel tu.

Majina ya kuitana mbu yalianza pale ambapo Zari alijisfia na kujiita tembo na kwamba hawezi  kufananishwa na mbu wanaouma nyumbani ndipo Hamisa alipokanusha kwa kujiiat mbu  na kwamba anaeweza kuua mtu kwa malaria.