Mama Diamond Amwaga Povu Kulinganishwa na Mobetto

Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi. Sandrah maarufu kama Mama Diamond amemwaga Povu zito baada ya mashabiki wa mtandaoni kumlinganisha na aliyekuwa mkwe Wake Hamisa Mobetto.

Sakata hilo lilitokea siku chache zilizopita baada ya Mama Dangote kuweka picha mtandaoni zilizomuonyesha akiwa amebebwa na Mume Wake Shamte ndipo mashabiki walimtuhumu kwa kumuiga Mobetto.

Siku za nyuma kidogo Mobetto aliweka picha zake na Mpenzi Wake Josh Adeyeye zilizomuonyesha wakiwa wamebebana kimahaba ndipo walipounganisha na zile za Mama Dangote na kumtuhumu kwa kuiga.

Katika mahojiano yake aliyofanya Global Publishers, Mama Diamond alimwaga Povu zito Baada ya kuulizwa kuhusu tuhuma hizo:

Unajua siwezi kujibu swali hilo la ajabu, kwani wewe ukibebwa unajisikiaje? Na hayo mambo ya Mobeto jijibu mwenyewe na uandike unachojisikia“.

 

Hamisa Mobetto Atumiwa Ujumbe Huu na Mpenzi Wake

Mwanamitindo na msanii wa Bongo movie Hamisa Mobetto ameonekana kuwa katika Penzi zito na Mpenzi Wake ambaye ni mcheza kikapu cha kulipwa nchini Marekani Josh Adeyeye.

Hamisa aliweka wazi mahusiano yake na Josh Wiki chache zilizopita baada ya kuposti picha na video zikiwaonyesha wakibebana kimahaba na hata kumpa uhusika wa Mpenzi Wake kwenye video ya nyimbo yake ‘Tunaendana’.

Siku ya jana Hamisa aliweka wazi kuwa amerudi nchini Tanzania Baada ya kukaa nchini Marekani kwa muda wa mwezi ambako alikuwa anapiga shoo katika miji mbali mbali.

Ingawa ni siku chache tangu Hamisa amuache Josh nchini Marekani wawili hao wameonekana kumisiana kwani Josh amemposti Hamisa kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuweka wazi kuwa amemiss na siku si nyingi atamuona.

Diamond Amtupia Dongo Hamisa Baada Ya Kumuanika Mpenzi Wake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amemtupia dongo zito aliyekuwa Mpenzi Wake na mzazi mwenzake Hamisa Mobetto Baada ya kumuanika mpenzi wake.

Wiki iliyopita Hamisa alimtambulisha rasmi Mpenzi Wake mpya anajulikana Kama Josh Adeyeye ambaye amekutana naye nchini Marekani alikoenda kwa ajili ya kupiga shoo.

Diamond ameibuka na kumtupia dongo zito Hamisa Baada ya Stori za Hamisa na Josh kupamba moto kola kona kwenye mitandao ya kijamii.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond ameandika:

Najua mwili wangu ni mtamu, na najua bado unanitamani, ila usije ukadanganyika, hauwezi kuhimili stress“.

Hamisa na Diamond waliachana miezi michache iliyopita Baada ya kukiri kuwa kwenye mahusiano kwa miaka kumi ambapo Hamisa alikiri kumuacha Diamond Baada ya kuona hana muelekeo naye.