Izzo Bisness Amefunguka Sababu Iliyompelekea Mpaka Kumwaga Machozi Hadharani

Mwanamuziki wa Bongo fleva Izzo Bisness amefungukia sababu iliyompelekea mpaka kumwaga machozi kwenye studio za Clouds FM siku chache zilizopita.

Izzo bisness alikuwa anafanya interview kwenye stesheni ya clouds fm katika cha kipindi cha XXL hot 3 ambapo alikuwa anatambulisha ngoma yake mpya ya Baraka lakini ghafla katika kuongea nakutoa shukrani zake kwa mwaka 2017 alipatwa na hisia na kuanza kulia.

Baada ya tukio hilo alizua gumzo huku watu wengi wakihohi labda kuna jingine lililosukuma hisia hizo. Kwrnye mahojiano na Millard  Ayo Izo Bisnesss alifunguka yafuatayo:

Jana nilikuwa Clouds nilipokuwa natambulisha wimbo wangu mpya niliomshirikisha Juma nature unaoitwa baraka na ni wimbo ambao nimeelezea Yale niliyopitia katika gemu na maisha yangu pamoja na familia yangu lakini kilichonifanya mpaka nikatoa machozi ni kwa sababu nilikuwa very emotional kwa sababu nilikuwa nakumbuka yale yote niliyopitia inawezekana nikawa sijapata mafanikio makubwa sana lakini inanirudisha nyuma na kukumbuka jinsi nilivyokuwa napitia makubwa na magumu zaidi ambapo nilikuwa najinyima ili tiu siku moja niishi maisha ya ndoto yangu”.

 

 

Izzo Bizness- Kolabo Ya Diamond na Rick Ross Itainua Muziki Wetu

Mwanamuziki na rapa kutoka Mbeya City Izzo Bizness amefunguka na kuongelea kolabo iliyofanyika baina ya msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz na rapa kutoka Marekani Rick Ross kuwa itasaidia kuinua muziki wetu wa Tanzania.

Izzo Bizness aliongea hayo kwenye mahojiano aliyoyafanya na kituo cha televisheni cha East Africa;

Kwanza Big up kwa Diamond na timu nzima ya Wasafi classic kwani matokeo ya kolabo iliyofanyika Kati ya Diamond na Rick Ross yatakuwa makubwa na pia uongozi mzima wa Diamond wanajitahidi kupush katika kutangaza mziki wa bongo fleva na ukiangalia Rick Ross ni msanii mkubwa sana na hiyo ni bahati kubwa sana si kwa mziki wa hip hop tu hadi bongo fleva na sanaa yote ya kuimba kwa ujumla Rick Ross ni msanii mkubwa duniani amafanya kazi na wasanii wakubwa sana duniani kwaiyo hii kolabo italeta attention kwa wale wanamziki wa nje kuangalia huyu msanii anatokea wapi na kuanza kujaribu kuangalia sasa soko la Tanzania linakuje wasanii na kadhalika, kwaiyo mi nahisi hii itasaidia sana na kwa kiasi chake kusaidia katika kuinua muziki wetu wa Bongo fleva”.

Ikiwa taarifa zaidi kuhusu kolabo hiyo haijawekwa wazi bado kama jina la wimbo, msanii gani kamshirikisha msanii gani na kadhalika lakini ni hatua kubwa kwa msanii wa Bongo fleva kama Diamond kuweza kushiriki sanaa yake na mwanamuziki mkubwa duniani kama Rick Ross kwani hatua hii ni kubwa na itafungua milango mingi kwa wasanii wengi.