Izzo Business- Siamini Katika Nguvu Ya Kiki Kwenye Sanaa

Msanii wa muziki wa hop hop nchini Izzo Business amefunguka kuhusu ukimya wake kwenye gems anapokuwa Hana nyimbo inayofanya vizuri kwenye vyombo vya habari lakini pia suala la Kiki.

Wasanii wengi wamekuwa wakitafuta kiki am app wamekuwa wakitengeneza skendo mbali mbali ambazo zinakuwa nje ya Sanaa ilimradi tu waendelee kuongelewa hasa kwenye mitandao ya kijamii.

Katika mahojiano yake na Gazeti la Risasi Vibes, Izzo Business alifunguka Baada ya kuulizwa sababu za kupotea kabisa anapokuwa hana nyimbo inayohit kwenye media:

Unajua kila mtu ana life style yake ambayo yeye anapenda kuishi na mara nyingi huwa mimi sipendi kuishi uongo, mimi napenda kuishi maisha yangu ambayo nayamudu siyo ya kujioneshaonesha kama sina kitu cha umuhimu au ulazima wa kufanya hivyo“.

Lakini pia Izzo alifunguka na kuweka wazi kuwa yeye sio mtu wa kutafuta Kiki na haamini sana kwenye Kiki Kiki za Sanaa:

Siamini sana kwenye kiki kwa sababu siku zote kazi nzuri inajiuza tu hata bila kiki. Unajua kiki ni ‘fifty fifty’ inaweza ikakupandisha unapotaka au ikakushusha tofauti na pale ambapo ulikuwepo na kila mtu ana mazingira na staili ambayo alianza sanaa yake kwa hiyo mimi kiki hapana kwakweli, kazi kama nzuri watu watasapoti tu ikiwa haijafikia kiwango, basi tutarudi studio kufanya kazi mpya“.

 

“Wema Awe Makini Kuna Watu Wanamuangalia”- Izzo B

Msanii wa muziki wa hip hop nchini anayetokea pande za Mbeya Izzo Business amefungukia sakata lianaloendelea hivi sasa na kushika headlines kwenye mitandao ya kijamii kumuhusu msanii wa maigizo nchini Wema Sepetu.

Wema Sepetu amefikishwa mahakani siku ya jana kwa tuhuma za kusambaza picha zake za faragha na mpenzi wake na kuziweka katika mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano na gazeti la Ijumaa, Izzo Business ameibuka na kumshauri Wema kuwa mwangalifu katika siku za mbeleni kwani haileti picha nzuri hasa kwa yeye ambaye ni kioo cha jamii;

Naweza nikasema awe makini sana kutokana na pozisheni ambayo anayo kwa sababu yeye ni brand, anafahamika sana, kuna watu wengi ambao yeye ‘anawa-inspire’ na wengi wanamtazama yeye na kama unavyojua siku hizi kwenye mitandao hadi watoto wa chini ya miaka kumi na nane wapo na wanam-follow Wema kwa sababu wanatamani kuwa kama yeye. Kwa hiyo ushauri wangu ni vitu binafsi kama vile vibaki kuwa binafsi tu, kujirekodi hukatazwi, weka katika sehemu ya siri ili uangalie wewe, lakini siyo mpaka kuvitoa nje siyo kitu kizuri”.