Mh Kikwete Ashtushwa na Habari za Kifo cha Godzilla

Moja ya viongozi waliowahi kuwa karibu sana na wasanii kipindi cha uongozi wake mh jakaya kikwete , amesema kuwa amepokea kwa mshtuko sana taarifa ya kifo cha mwanamuziki Godzilla kwa sababu alikuwa moja ya vijana wadogo  mwenye ndoto kubwa maishani.

mh kikwete aliongea maneno hayo huku akiambatanisha na picha yake aliyowahi kuipiga akiwa na msanii huyo miaka ya nyuma.

Raisi Mstaafu Kikwete Ampa Onyo Kali Diamond Platnumz

Raisi mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakarta Kikwete amempa wosia mzito Msanii ambaye ni staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Gazeti la Ijumaa linaripoti kuwa Raisi Kikwete alimuita Diamond nyumbani kwake jijini Dar na kumpa wosia mzito ambao uligeuka gumzo huku staa huyo akikomaliwa juu ya mambo matatu ndani yake.

Diamond ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) alifunguka juu ya wosia huo kama ifuatavyo; “Nilipokuwa Mwanza (kwa ajili ya Tamasha la Wasafi), Rais mstaafu Jakaya Kikwete alinipigia simu na kunitaka niende nikamuone haraka”.

JAMBO LA KWANZA “Baadaye, nilikwenda nyumbani kwake (JK) jijini Dar. Pamoja na mambo mengine, nikiwa pale, kitu cha kwanza kabisa alinishauri nioe kwani umri unaruhusu (Diamond ana umri wa miaka 30 sasa). “Aliniambia ni muda muafaka kuoa na kutulia,” alisema Diamond na kuendelea:

JAMBO LA PILI “Pia alinionya juu ya kuposti video na picha kwenye mitandao ya kijamii zikionesha nikitandaza pesa mezani. “Hayo aliyasema baada ya mimi kuposti video kwenye Instagram ikimuonesha Tanasha (mpenzi mpya wa Diamond) na mimi tukiwa hotelini nikihesabu maburungutu ya pesa juu ya meza wakati Tanasha akipiga ‘selfie’ kwa kutumia simu janja.

“Rais huyo mstaafu aliniambia jambo hilo nililofanya halikuwa sahihi ukitegemea kwamba kuna watu hawana uwezo kabisa wa kimaisha ambao watajisikia vibaya kuniona mimi nikijionesha nina pes.

JAMBO LA TATU “Aliniambia niwe makini na mambo ninayoyafanya kwani mengine yanaweza kunijengea chuki kwa watu.

Aliniambia anaweza kuja mtu mbaya kunipongeza kwa mafanikio au jambo lolote, lakini siwezi kumjua kwani atakuwa anakuja mbele yangu akinichea usoni, lakini moyoni ana chuki.

Kwa upande mwingine aliniambia ninaweza kupata matatizo ya kipesa, nitakapomfuata mtu mwenye chuki na mimi ataishia kunipa pole tu usoni, lakini ndani ya moyo wake atakuwa na furaha, hapo nitakuwa nimepata matatizo kwenye maisha yangu”.