Kalala Junior Adaiwa Kuvuruga Ndoa Ya Uwoya na Dogo Janja

Msanii wa muziki wa dansi nchini Hamza Kalala ‘Kalala Junior’ anadaiwa kuwa chanzo cha mvurugano ulioikumba ndoa ya staa wa Bongo movie Irene Uwoya na Dogo Janja.

Global Publishers wanaripoti kuwa taarifa zinazosambaa Kwenye mitandao ya kijamii ni kuwa ndoa ya Dogo Janja na Uwoya imeingiwa doa na inasemekana chanzo ni Kalala kwani Uwoya amemzimikia vibaya mno Msanii huyo kiasi cha kumuhonga mizawadi kibao.

Baada ya kunasa tetesi hizo kutoka kwa chanzo cha kuaminika, gazeti la Risasi Vibes ilimtafuta Kalala ili aweke wazi juu ya madai hayo ya kuhongwa na kuivuruga ndoa ya Uwoya huyo na Dogo Janja.

Ni kweli nimeyasikia hayo maneno. Hata kwenye mitandao nimeona, lakini si kweli kabisa na nikwambie tu, tangu yaanze kusemwa yananivurugia hata kwenye uhusiano wangu.

Nina mtu wangu ninampenda na sipo na Uwoya ingawa ni rafiki yangu na mtu ambaye tunafahamiana”.

Baada ya kupata ukweli kutoka kwa Kalala Junior GPL lilimsaka Uwoya ili kusikia ukweli kutoka upande wake lakini hakuweza kupatikana kwani alikuwa nje ya nchi (Dubai) na Dogo Janja alipotafutwa alikataa kuongelea lolote kuhusu ndoa yake.