“Sina Habari na Mambo Ya Ndoa”- Linah Sanga

Mwanamuziki wa Bongo fleva mrembo Linah Sanga amefunguka na kuweka wazi kuwa hivi sasa hana mpango wa kuolewa na wala hawazi kuhusu mambo ya ndoa.

Linah amefunguka kuwa maisha ya ndoa kwa sasa hayafikirii na badala yake anatamani kuona muziki wake unampa heshima kwanza.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la DIMBA, Linah alisema, licha ya wanawake wengi kutamani ndoa lakini kwake inekuwa tofauti na badala yake ameelekeza nguvu zaidi kwenye kazi zake.

Mimi ukiniuliza mambo ya ndoa kwa sasa ni ngumu kueleza.. niulize muziki wangu unakwendaje au kuhusu mwanangu”.

Linah amezaa Mtoto mmoja na mwanaume ambaye alikuwa kwenye mahusiano naye ya muda mrefu aitwaye Shaban Mchomvu ambaye amezaa naye Mtoto mmoja wa kike anayeitwa Tracey Paris.

Linah Sanga Azidi Kukwepa Tetesi Za Kumwagwa na Baba Watoto Wake

Mwanamuziki wa Bongo fleva nchini Linah Sanga amezidi kukwepa tetesi za kuwa ameachana na Mpenzi na mwanaume aliyezaa naye Mtoto Wake wa kwanza Shaban Mchomvu.

Kwa miezi kadhaa sasa kumekuwa na tetesi kuwa Linah na baba watoto wake wameachana Baada ya Shabani kuchoshwa na maisha ya kimuziki anayoishi Linah ikiwemo mavazi ya ajabu.

Lakini Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi Enews cha EATV,  Baada ya kuulizwa kuhusu taarifa hizo Linah amekuja juu na kuwataka watu wafatilie muziki Wake na sio maisha yake binafsi.

Sidhani kama mashabiki zangu wanatakiwa kufahamu kuhusu maisha yangu binafsi, wanachopaswa kukifahamu ni muziki wangu tu kwaiyo siwezi kuzungumzia hilo”.

Linah ametangaza kutoa wimbo wake mpya hivi karibuni na kuwataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kwani video ya wimbo huo imeshakwisha kamilika.