Mainda Aitupia Lawama Mitandao Ya Kijamii Kwa Sakata La Msiba Wa Patrick

Msanii Mkongwe wa filamu za kibongo (Bongo movie) Ruth Suka maarufu kama Mainda, ametupa lawama zake zote kwa mitandao ya kijamii baada ya sakata la mazishi ya mtoto Patrick.

Mainda amefunguka na kudai isingekuwa uwepo wa timu timu Kwenye mitandao ya kijamii basi anaamini mtoto Patrick angezikwa vizuri bila ya mashabiki kuingilia Familia ya watu.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers. Mainda alisema anaamini watu wa mitandaoni wamechangia kwa kiasi kikubwa kuweka taarifa za upotoshaji kati ya Muna na mumewe Peter ambazo zimesababisha wawili hao washindwe kuelewana haraka.

Jamani hivi ni vitu gani? Ndiyo maana mimi sipo kwenye mitandao nina sababu kubwa sana. Kuna upotoshaji wa hali ya juu na kama isingekuwa mambo ya matimu haya kusingetokea mvutano mkubwa uliokuwepo na kusababisha mambo mazito kwenye msiba wa mtoto asiyekuwa na hatia kabisa“.

Mvutano mkubwa ulitokea hasa kwa sababu ya mgawanyiko wa kifamilia lakini baadae walifikia uamuzi sahihi na siku ya Jumamosi mtoto Patrick alipumzishwa kwa amani.