Wolper amepata mchumba mwingine baada ya Harmonize?

Muigizaji wa filamu Wolper Stylish anaonekana kuwa amepata mchumba mpya baada kuachana na Harmonize ambaye anatarajia mtoto wake wa kwanza na mrembo wake mpya wa kizungu.

Wolper Stylish
Wolper Stylish

Kuachana kwa wawili hawa kuliwashtua mashabiki wao ambao walikuwa wakitarajia harusi kulingana na walivyokuwa wakipendana. Hata hivyo Harmonize alidhibitisha kuwa uhusiano wao ulikuwa umeisha na sasa alikuwa na mchumba mpya.

Hata hivyo Wolper alikaa kimya hadi Jana alipoandika ujumbe ambao umewaacha wengi wakisema kuwa kunauwezekano kuwa amepata mwanaume ambaye ameituliza roho yake sasa.