Miss Tanzania Diana Edwards adai kujiunga na filamu za Bongo

Diana Edward ambaye ni Miss Tanzania 2016/7 ameonyesha uwezo wa kujiunga na filamu za Bongo kama Wema Sepetu. Mrembo huyu ambaye amepata sifa nyingi baada ya kuibuka mashindi wa Miss Tanzania kwa sasa anaolea kufanya mambo na filamu.

Mrembo huyu alifunguka kwenye kipindi cha Twenzentu cha Times FM na kusema kuwa kila kitu kimepangwa na kile anachongoja ni kuanza kuigiza.

Aliendelea kwa kusema kuwa yeye amekuwa akiigiza kwa muda mrefu kwa hivyo haitakuwa ngumu kufanya filamu yoyote. Alisema,

“Kila kitu kipo tayari, nimeshafanya mazoezi sasa hivi nasubiria mambo yangu yakikaa sawa nianze kutengeneza. Napenda action movie kwa sababu am so addicted in action movie, staki kusema mengi sana kwa sababu nasubiria maamuzi kutoka kwa meneja wangu itakuwaje, kwa hiyo msubiri. Mimi nilikuwa naigiza kuanzia muda mrefu ingawa sikutoa movie yoyote.”