Moni Awatolea Povu Zito Mashabiki Zake

Msanii wa Bongo fleva anafanya miondoko ya kurap Awadhi Mtezo maarufu kama Moni Central Zone amewatolea povu zito mashabiki zake ambao wamemtuhunu kwa kutegemea kiki ndio afanye muziki.

Kumekuwa na trend kubwa kwa hivi sasa kwa wasanii wa Bongo fleva kupenda kiki yaani msanii anakuwa haoni kama muziki wake utafanya vizuri bila kiki na kabisa anapanga kabla hajatoa wimbo lazima atengeneze kiki wakuusindikiza.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Star Showbiz, baada ya kuulizwa kuhusu komenti hizo za mashabiki kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram, ambao walidai hivi karibuni alipokuwa anataka kupushi ngoma yake mpya ya Mwaah, alitumia kiki ya ugomvi na mwanamuziki Roma alifunguka hivi:

Hata siku moja sitegemei kiki. Muziki wangu ni mzuri na unajiuza wenyewe. Kikubwa kilichokuwepo kwa sababu nilikuwa karibu na R.O.M.A, mambo yalikuwa hayaendi vizuri kwa sababu alikuwa anaonekana yeye tu na si mimi, lakini baada ya kila mtu kuchukua time yake, kwa sasa naonekana mwenyewe na si kwamba nategemea kiki”.