Msaga Sumu Awatahadhalisha Wanawake Wanaomshobokea.

Msanii kinara wa muziki wa singeli nchini  Selemani Jabiri maarufu kama Msaga Sumu amefungukia swala la tabia za  wanawake wanaokuwa wakisumbua wasanii katika mitandao ya kijamii na hata kutafuta namba zao za simu kwa ajili ya kuwataka kimapenzi bila kujua kuwa wasanii wengine wanafamila zao tayari.Msaga Sumu anawahasa  wanaokuwa wanamsumbua na wanamtaka kimapenzi kuwa yeye ana mke na watoto wawili hivyo anawaomba wamuache kabisa kwa sababu anaipenda familia yake.

Msaga Sumu ambae alipata kujulikana zaidi na wimbo wake wa  mwanaume mashine amesemakuwa amekuw akisumbuliwa sana na wanawake kimapenzi lakini anachowashangaa ni kwamba wapo wanaojua kuwa yeye anafamilia yenye mke na watoto hivyo anaomba sana kutokusumbuliwa sana.

Imekuwa kero sasa , ninachoweza kuwaambia tu ni kwamba  wanawake waache kabisa kunishobokea shobokea  kwanza watambue kuwa nina familia lakini pia wajue kuwa ninaipenda sana familia yangu  na ninatimiza miaka nane ya ndoa yangu kwa sasa. Na nina watoto wawili Inshallah Mungu kanijalia. Alifunguka Msaga Sumu

Hata hivyo msanii huyo wa singeli akiendelea kuongelea swala lake la muziki anasema kuwa kwa sasa ameshajipanga na anakaribia kuzindua mwanaume mashine .

kwa sasa najipanga kuzindua mwanaume mashine  ndani ya dar live soon ntatangaza  kuwajulisha kuhusu hilo.  Alimalizia Msaga Sumu

Wasanii wengi wamekuwa wakilalamika hasa wa kiume kuwa wamekuwa wakifatwa dm kuuliza kuhusu maisha yao ya kimahusiano na hata wanawake wengine kuwataka kimapenzi , ukiachana na Msaga Sumu wasanii wengi wa kiume wamekuwa wakifungukia swala la wanawake kuwataka kimapenzi hivyo wanaomba kupunguziwa shuruba hizo kwa sababu wengine wana familia.

 

Ben Pol Amfananisha Msaga Sumu Na Dr.Remmy

Ni wasanii wachache sana wanaokubali kazi za wasanii wenzao tena hasa wanapokuja katika swala zima la kazi za musiki kwa sababu wengi wanaamini kuwa ili kufanikiwa kimuziki basi lazima kuwe na ushindani.Hii imekuwa tofauti kwa msanii wa Bongo Fleva anaejulikana kwa kufanya vizuri na kupewa jina la king of Rnb , msanii Ben Pol ambae ameibuka na kuusifia sna muziki wa msanii mwenzie Msaga Sumu.

Akiongea na kipindi kinachorushwa na Clouds Radio cha XXL, Ben Pol ambae kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake cha ‘kidume’ alichomshirikisha mwanadada mrembo kabisa kutoka Nigeria Chidinma Chikere, Ben Pol anasema anavutiwa sana na ufanyaji muziki wa msanii mwenzie Msaga Sumu.

Sijui kama Msaga Sumu ni upcoming artist au sio lakini  napenda sana muziki wake na jinsi  anavyokuja , ana-flavor , yake kama Dr.remmy  au sound flani hivi  ya kitofauti sana, na ninamuona jinsi atakavyofika mbali katika muziki wake’ alifunguka Ben Pol kuhusu Msaga Sumu

Ben Pol anaendelea kumuongelea Msaga Sumu na kusema kuwa ni msanii mwenye kipaji cha kuweza kubadilika badilika na kuimba nyimbo zenye radha tofauti tofauti”Alafu anaweza kubadilikabadilika kila mara, mara nyingine anaweza kuimba zilipendwa, au anaweza kuimba singeli, kama oya oya oya  lakini ni msanii mwenye vitu vingi sana” aliongezea ben pol

Msaga Sumu ni mmoja wa wasanii wanaochipukia na kufanya vizuri katika game la muziki hasa katika style hii mpya ya muziki wa kisingeli iliyopo sokoni kwa sasa, hata hivyo Msaga Sumu anaweza kuita mwanzilishi wa kisingeli na ndiO msanii alijitaidi hata kuhamamsisha wasanii wengine wadogo kufanya muziki wa kisingeli hivyo  kusababisha kukua kwa kisingeli.Msaga Sumu kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake cha singeli kinachojulikana kama  “mwanaume mashine” inayopendwa sana hadi na watoto kutokana na style yake ya kuimba na kucheza huku ikitaja baadhi ya majina maarufu ya wacheza mpira na timu kubwa nchini , hapo mwanzo alifanya vizuri na kibao cha “unanitega shemeji’.

Msaga Sumu Awashauri Wasanii Wa Singeli Kuwa Na Heshima

Msanii mkali katika muziki aina ya singeli Msaga Sumu  amefunguka na kuongea na  baadhi ya wasanii wenzie  wanaokaa  na kudharau wasanii wenzao. Msaga Sumu ambae anafanya vizuri katika aina hiyo mpya ya muziki na  imekuja kwa kasi isiyo ya kawaida na kupendwa na watu wengi ameamua kuyaongea hayo kama ushauri kwa wasanii wenzie.

Alipokuwa akiongea katika telesheni ya EATV, Msaga Sumu  aliamua kuongea maneno hayo baada ya kusikia baadhi ya maneno kutoka kwa wasanii wenzie ambao kwa muda wamekuwa wakimsema yeye vibaya, msaga sumu anasema kuwa wasanii wenzie wa singeli wamekuwa wakimwambia yeye hajui chochote kuhusu muziki huo wa singeli.

“Wasanii  wa singeli mimi naamin wananiponda sana , tena nikikaa kimya hivi ndo wanasema nimefulia kabisaaaa,kumbe mwenzao nipo najitungia sheria zangu huku nikiwaangalia wao , lakini huwa nawaambia ukweli kuwa  siki zote kwenye muziki  ukiwa na heshima  unaweza kufika mbali , kwa kuwa heshima ndio kila kitu” aliongea Msaga Sumu

Hata hivyo Msaga sumu anaonekana kukerwa na baadhi ya wasanii wenzie wa singeli ambao wamekuwa na tabia ya  kujiona vichwa na kutokuheshimu wenzao pale tu wanapotoa wimbo mmoja ukafanya vizuri basi wanajiona ndio wameshafika katika muziki na kuanza kuvimba “hawa wasanii wa singeli wengi watafeli  muziki kwa sababu heshima hawana, wanajifanya wanavimba vimba na nyimbo moja tu walizokuwa nazo’ ameongezea Msaga Sumu

Msaga Sumu ambae amekuwa akiaaminika kuwa yeye ndio muanzilishi wa muziki huu mpya wa kisingeli ambao unatamba kwa sasa akiutoa katika ngoma za mitaani zinazijulikana kama vigodoro na kufanya wasanii wengine wenye vipaji vya muziki huo kujitokeza.Hata hivyo kwa sasa muziki wa kisingeli umekuwana na wasanii wengi na wanafanya vizuri huku pia mashabiki wakiupokea vizuri sokoni.Haya basi akiwa kama muanzilishi wa muziki huu ameona sio vibaya kuongea na wasanii wenzake ili kufanya aina hii ya muziki usiyumbeyumbe.baadhi ya wasanii wengine wanaofanya vizuri katika muziki huo ni pamoja na Dullah Makabila ,Manfongo na Shollo Mwamba.