Nai Atoa Jibu Hili Baada Ya Tuhuma Za Kuazima Nguo Kwa Linah

Video vixen maarufu na Mpenzi wa Msanii wa Bongo fleva Centro Zone Nai au maarufu kama Nai Official amefungukia tuhuma za kumuanika nguo Msanii mwingine wa Bongo fleva Linah Sanga.

Nai amewatolea povu zito mashabiki walioanzisha taarifa hizo za uongo na  kuwataka wafunge midomo yao kwani hawajui wanachokiongelea kwani yeye sio mtu wa kuazima nguo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Nai alisema hawezi kuazima nguo kwa mtu yeyote kwani ni bora arudie nguo lakini siyo kuazima, kilichotokea kwake na Linah ni kwamba nguo zimefanana ila kila mtu amenunua kwa wakati wake na ndiyo maana alifanya utani kumshukuru Linah mtandaoni kwa kumpa gauni kwa sababu yamefanana ila watu wakadhani ni kweli amemuazima.

Hizo ni dharau sasa ina maana ndiyo nimefulia kiasi hicho mpaka nishindwe kununua gauni? Nilijua tu watu wataongea ndiyo maana nikafanya makusudi kumshukuru Linah kama amenipa ila nilifanya utani kwa sababu magauni yamefanana, yeye lake alivaa kwenye shoo Iringa mimi nimevaa kwenye bethidei ya Wolper, sasa kama kiwanda kinatoa nguo moja watu wanataka tufanyeje”.