Nay Wa Mitego anahofia maisha yake Sasa

Rapper Nay Wa Mitego ameewacha wengi wakimhofia maisha yake baada ya ujumbe aliouandika kwenye mtandao wake wa Instagram. Ujumbe huu umekuja wiki moja baada ya rapper huyo aliwekwa ndani na jeshi la polisi baada ya kuachia wimbo wake mpya ‘Wapo’.

Kulingana na ubuyu mitandaoni, wimbo huu ukikuwa ukichana serikali ya Magufuli hata hivyo Rais wa Tanzania Magufuli alitoa amri msanii huyo kuachiwa kwa kwa kusema wimbo wake haukuwa na matatizo yoyote.

Hata hivyo, Nay wa Mitego sasa hivi anasema kuwa anahofia maisha yake kwani anahisi kwamba kuna watu wanaotaka kumpoteza. Kupitia Instagram aliandika kusema

“Usalama wa maisha yangu umekua mdogo kwasasa, Wanapanga kunipoteza ikibidi nisiwepo kabisa kwenye hii dunia. Nipo tayari kwa chochote wanacho panga kufanya Coz sijajipanga kupambana nao, Mimi ni mwana muziki si vingine. Kwa chochote kitachotokea familia yangu itakua na chakuongea. Siwezi kuhama nchi wala kukimbia nitafia hapa hapa. Na siko tayari kupindisha chochote.! nyie Ndo mtanilinda. Sina Mlinzi na sitarajii kua na mlinzi. OnlyGod??#Wapo,”

Haijulikani ni nini kilichomfanya kuhisi hivyo, lakini tunafuatilia kusikia atachokisema hivi karibuni.