Ney Wa Mitego aongelea bifu za wasanii

Kumekuwepo na bifu nyingi sana zinazoendelea katika mitandao dhidi ya wasanii wa Bongo Fleva na Bongo Movies, kwa ujumla katika tasnia ya sanaa ,bifu hizo zimekuwa zikiibuka bila kujali ukongwe au upya wa wasanii wanaojiingiza katika bifu hizo,  huku baadhi ya sababu za mifarakano hiyo kutokujulikana kwa uhalisia wake, kuna baadhi wanaogombana kwa sababu ya wivu, wapo wanaogombana tu ili kupata kiki katika tasnia , ila wapo wanaofanya hivyo ili kukuza game la kazi zao.Kwa kiasi kikubwa katika tasnia, Bongo Fleva imekuwa ikiongoza katika kuzusha bifu baina yao ,huku wengine wakiingia hadi studio kuandika wimbo kwa ajili ya kujibu yale wanayotuhumiwa na wasanii wenzao.

Msanii wa Bongo Fleva Emmanuel Elbariki Munisi maarufu kama Ney Wa Mitego “True boy” anaetamba kwa sasa na kibao chake kipya cha “maku” , lakini pia ni moja ya wasanii ambao hujikuta matatani na wasanii wenzie  kwa sababu ya nyimbo nyingi anazotoa huku akitoa madongo  kwa baadhi ya wasanii au yanayotokea katika jamii kwa ujumla.

Ney Wa Mitego anasema kuwa anaposikia wasanii wana bifu huwa anawaza vitu viwili ‘huwa nawaza chachu kwenye game kati ya bifu yao, pia nawaza biashara wanayoenda kuifanya ” hivyo uwa anaangalia je ilo bifu yupo nani na nani na akishaajua uwa anafanya tathmini ya bifu ilo kama kama itakuwa ni biashara nzuri au la. Ney anasema kuwa endapo atagundua kuwa bifu ilo sio la kibiashara au linatoka moyoni basi kwake bifu ilo huwa sio zuri.”Game zuri ni lile linaloleta  challenge katika muziki ,tuwe na ushindani wa kutoa nyimbo nzuri, au tuwe na ushindani wa kujaza watu kwenye show”Aliongezea Ney.

Ney Wa Mitego anaongezea kuwa bifu litakuwa zuri kama unasikia mtu katoa ngoma na wewe unatoa ngoma, msanii huyu kanunua gari na wewe unanunua nyumba, wasanii wawe na bifu la kuwaasha mashabiki, lakini kama bifu ilo litakuwa lenye kuleta chuki na kinyogo  inayoanzia moyoni huwa sizisapoti na sizipendagi.

Ney Wa Mitego Ahofia Kuongelea Hali ya Usalama Nchini

Msanii wa Bongo fleva nchini Ney wa Mitego anayejulikana kwa uwezo wake wa kupaza sauti na kuongea ukweli kuhusiana na mambo mbalimbali  katika jamii kwa mara ya kwanza amefunguka na kuhusu hali ya usalama ilivyo hapa nchini kufuatia mauaji ya na shambulio la risasi la Tundu Lissu ambalo limetikisa nchi nzima.

Ney amesema ingawa wasanii ndio watu wakipaza sauti zinaeleweka kwa wingi hata kwa wasiofatilia siasa, lakini ameona bora ayaache mambo hayo kwa  wenyewe wanasiasa kutokana na uoga aliokuwa nao.

Ney ameendelea kufunguka kuwa anatamani kuongea lakini kutokana na hali ilivyo kwa sasa anahofia usalama wake na familia yake kwani hata familia yake humkalisha chini na kumuonya na yeye kuamua kukaa kimya, na kuwaachia wanasiasa waendelee kupambana wenyewe.