Nay Wa Mitego Arusha Dongo Baada Ya Listi Za Wasanii Watakaoperfom Kuwekwa Wazi

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa mitindo yake ya kuchana Emmanuel Elibariki maarufu Kama Ney Wa Mitego ameibuka na kutoa Povu zito Baada ya listi za wasanii watakaoperfom kuachiwa.

Wikiendi ijayo itakuwa na burudani kila kona kwani maya maisha kadhaa yatafanyika katika Mikva tofauti tofauti.

Matamasha hayo moja linaitwa Fiesta ambalo litafanykia hapa Dar Es Salaam, lingine ni Wasafi Festival litakalofanyika Mtwara na la mwisho ni lile litakalofanyika Kahama ambapo Alikiba ataenda kuperform na kundi lake la Kingsmusic.

Ney wa Mitego  amefunguka na kusema haya:

Mmh Nasubiri Kuona List Ikiendelea But Mmh. Awa Mbona Hawana Maajabu.?! Waimba Bure Wote Ninao Waona Apa?? Hawapatagi Show Ata Za Bure Awa. Oyaa Nataka Kuona List Ya Wasanii Heavy Sio Awa Wasio Julikana Ata Makwao Kama Wanaimba?? Msiniangushe Wazeeeeeeeee.! …….
#Tar24. Wanangu Wa Dar Hakikisheni Mnaenda #Leader‘s Kwa Wingiii. Wanangu Wa Mtwara Hakikisheni Mnajaa Pale #Nangwanda. Na Machizi Wangu Wa #Kahama Inabidi Mkajae Pale #UwanjaWaTaifa.
Mkifika Sehemu Zote Wapeni Salamu Zangu #HakunaMaishaMagumu“.

 

Muziki wa Bongo Fleva Mwisho ni 2018:Nay wa Mitego

Msanii Ney wa Mitego maefunguka na kusema kuwa muziki wa bongo fleva unakaribia kufa na wanaoufanya ufe ni watu wakubwa ambao hawataki kusahaurika.Ney wa mitego anasema kuwa muziki huu unapotezwa na watu wenye mamlaka makubwa serikalini.

Ney wa Mitego amesema kuwa muziki wa bongo fleva unaenda kupotea kama ambavyo inavyopotea sanaa ya bingo movie na wasanii wake wataanza kupotea pia.Hayo yote yamesemwa na Ney wa Mitego baada ya kuwepo kwa mjadala mkubwa wiki hii uliohusiha watangazaji wa Clouds radio na Baraza la Sanaa pamoja na Naibu Waziri wakizungumzia matatizo ya wasanii hasa sakata la kufungiwa kwa wasanii na nyimbo zao.

Katika mjadala huo watu wengi waliuliza ili kutaka kujua sheria na taratibu zinazotumiwa na baraza ili kufungia nyimbo na msanii  na huku wakihoji kwanini BASATA  wamekuwa wakisimamia kuhusu maadili tu na kuacha vitu vingine.

Hata hivyo majibu yaliyotolewa na Baraza pamoja na Naibu waziri hayakuonekana kuwaridhisha wasanii kwa sababu hata baada ya majadala huo bali kulikuwa na malalamiko juu ya maelezo yao.

Kwa mahojiano ya leo, mtakuwa mmeelewa tatizo ni nini, naona mwisho wa huu muziki wa bongo fleva  utakwamia hapa 2018.mkubwa atabaki kuwa mkubwa tu na mdogo ataendelea kuwa mdogo , na tusivyo  na umoja tutaendelea kuwa wadogo na tunakoelekea ni tunaenda kule walikoenda ndugu zetu bongo movies.

Nay wa Mitego: Bongo Fleva Itakufa na BASATA na Serikali Ndio Chanzo

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nay wa Mitego amefunguka na kusema Muziki wa Bongo fleva uko mbioni kupoteza na kufanya kama Bongo fleva na hii yote inasababishwa na serikali na BASATA.

Wiki chache zilizopita Nay wa Mitego alikuwa mmoja kati ya wasanii waliofungiwa nyimbo kuchezwa kwenye vyombo vya habari kwa madai kuwa haziendani na maadili ya Tanzania.

Maoni hayo ya Nay wa Mitego  yalikuja baada mjadala mzito kati ya Naibu Waziri wa habari Juliana Shonza na viongozi wa BASATA walipokuwa wanajibu maswali mbali mbali kuhusu hatua wanazoendeela kuchukua dhidi ya wasanii hao.

Kwenye mjadala watu wengi waliuliza maswali kuhusiana na vigezo vya kufungiwa kwa wasanii na nyimbo zao huku wengine wakihoji kwanini BASATA wanasimamia kigezo cha maadili pekee? lakini majibu kutoka BASATA hayakuwaridhisha wala kuwaingia vichwani baadhi ya wasanii akiwemo Nay Wa Mitego.

Nay wa Mitego alitumia ukurasa wake wa Twitter na kuweka ujumbe wake huo wa kukata tamaa juu ya Bongo fleva:

Kwa mahojiano yao leo mtakua mmeelewa tatizo ni nini.?! Naona mwisho wa huu muziki, Umekwamia hapa rasmi 2018. Mkubwa atabaki kuwa mkubwa na mdogo ataendelea kuwa mdogo. Na tusivyo na umoja tunaenda walikoenda ndugu zetu Bongo Movie“.

Nay wa Mitego:Sasa Hivi Sitaki Kubishana na Mtu Nataka Kufanya Kazi Tu

Msanii Ney wa Mitego amefunguka na kusema kuwa kwa upande wake huu sio muda wa yeye kugombana au kushindana na watu bali sasa hivi ameamua kufanya kazi kwaio kwa wale wanaosema yeye hatokaa hawajibu bali atawajibu kwa kazi.

Alipokuwa akiongea katika kipindi cha Planet Bongo, Ney wa Mitego ambae sasa hivi anafanya vizuri na kibao chake cha mikono juu amesema kuwa kwa sasa amekuwa akihangaka sana ili kukuza na kuupeleka muziki wake mbele na sio kitu kingine.

Sasa hivi sitaki kujibizana na mtu kabisa kabisa , this time nataka kufanya kazi ili niupeleke muziki wangu mbele kwa watu wangu.miaka miwili  mitatu nilikuwa nafanya kazi na hivi vitu vingine nilikuwa ninaviweka vinakuja nyuma tu.tis time nikiona mtu anaingia na aantaka kuleta kelele na mimi basi ninampisha tu akaendeleae na vitu vyake maana huo sio muda wangu.

Wimbo wa Ney wa Mitego mpya umekuwa ukifanya vizuri na hata kupugwa katika madaladala na bodaboda ambapo Nay wa Mitego anasema kuw akiwa anafikiria kufanya mzuiki huo icho ndicho alikuwa anakitaka kwaio sio mbaya kwake.

hivi juzi kati, Nay wa Mitego aliingia katika mgogoro na Godzillah kutokana na wimbo wake huo mpya ambao Godzillah aliupondea sana wimbo huo.

Ney wa Mitego Amefunguka Baada Kumtabiria Diamond Kushuka Kimuziki

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Ney wa Mitego amefunguka na kuongelea jambo ambalo lilimfanya atengeneze headlines kwenye mitandao ya kijamii siku za nyuma kidogo kuhusu Diamond kushuka kimuziki.

Ney wa Mitego alishangaza watu wengi alipoanza kumponda Diamond ukitegemea wamekuwa marafiki kwa kipindi kirefu na hata wamefanya mziki kwa pamoja ambapo amemshirikisha kwenye nyimbo yake iliyofanya vizuri sana miaka ya nyuma ‘Muziki gani’.

Hivi karibuni kupitia mtandao wa Instagram, Ney aliweka picha ya mnyama simba akionekana akiuwawa kikatili jambo lilitafsiriwa kuwa yule ni Diamond kutokana na tayari inajulikana jina jingine la Diamond ni Simba akimaanisha yeye ni mfalme wa mwituni.

Kwa kuweka picha ya Simba akiuwawa ilisemekana kuwa au ilitfsiriwa kuwa Ney wa Mitego alikuwa anatabiri Diamond kushuka kimuziki. Kwenye mahojiano aliyofanya Times Fm katika kipindi cha The playlist Ney amesema hakukusudia jambo lolote baya ama hakua na nia mbaya dhidi ya Diamond kwa sababu ni mshkaji wake.

Diamond ni mshkaji wangu tumefanya kazi kubwa sidhani kama imefika hatua ya sisi kuwa maadui kiasi hicho na siwezi kumuombea mabaya kiasi hicho lakini tunaona changamoto anazopitia. Nilijua tu ile picha wabongo kila mmoja ataongea la kwake lakini sina tatizo na Diamond lakini hata kama lipo basi tutalimaliza lakini ile picha ilikuwa haimuhusu”.

 

NAY Wa Mitego Afunguka Kuhusu Nini.

Msanii wa bongo fleva nchini Ney wa Mitego amefunguka na kutilia mkazo swala la watu kusambaza maneno kuwa yeye na msanii mwenzake anaekuja vizuri katika swala la muziki, nini wamekuwa na  mahusiano ya mapenzi kwa muda mrefu,ney wa mitego anasema kuwa watu wanaosambaza taarifa hizo hazina ukweli wowote lakini anashindwa kuendelea kuongea kwa sababu watu walishaweka maneno midomoni tayari.

Siku za nyuma , Ney wa Mitego na Nini walisemekana kuwa katika mahusiano ya kimapenzi ya muda mrefu na kusemekana kuwa sababu kubwa ya meneja wa Nini (Daxo Chali ) kuvunja mkataba nao ni kwa sababu Ney wa Mitego amekuwa akim-control na kumfanya mwanadada huyo kushindwa kufanya kazi  vizuri .

Ney wa Mitego anasema kuwa tatizo la mashabiki wengi hata wakiambiwa nini wanakuwa tayari wameshajiwekea maneno yao midomoni kwaio hakuna haja ya kusema neno lolote la kumfanya mtu uyo aamini.

Unajua ukiwaambia watu kuwa ni marafiki tu hawakuelewi,ukiwaambia kuwa unafanya nae kazi wala hawatakuelewi  basi na mimi nafikiri kwa sasa imetosha , jibu ninalo moyoni mwangu. -Alisema Ney Wa Mitego.

wawili hao hivi karibuni walitoa wimbo mpya unaoitwa Niwe Dawa,ambapo baada ya wimbo huo watu wengi walidhani kuwa nini kwa sasa atakuwa chini ya lebel ya ney wa mitego lakini nini mwenyewe alikanusha habari hizo na kusema kuwa kwa sasa hana menejiment yoyote

Siwema Wa Ney Afunguka Mahusiano Yake na Mtoto Wake

Mwanadada mrembo ambae alishawahi kuwa na mahusino ya kimapenzi na msanii Ney wa Mitego  na kubahatika kupata mtoto mmoja wa kiume anaejulikana kwa jina la Siwema, amefunguka kuongelea mahusiao yake na mtoto wake huyo wa kiume ambae kwa sasa anakaa kwa Ney wa Mitego na amekuwa akilelewa na mama mzazi wa Ney wa Mitego tangu wawili hao walipoachana.

Ney wa Mitego na Siwema waliachana kama miaka miwili iliyopita huku sababu kubwa ikiwa ni ufuksa  wa mwanamke huyo na kuandamwa na kesi zilizompelekea kuwekwa rumande mara kadhaa hiyo kumfanya ney wa mitego kuamua kumchukua mtoto huyo ili aweze kulelewa akiwa kwao.

Ney wa mitego akiwa na mtoto wake wa kiume.

Hata hivyo habari za hapa karibuni zilikuwa zikisema kuwa tangu wawili hao waweze na Ney wa Mitego kumchukua mtoto mwanamke huyo hajawahi kuonana na mtoto wake kwa sababu hakuna mahusiano mazuri kati yao.Akikanusha hilo Siwema amesema kuwa sio kweli kuwa hajawahi kumuona mtoto huyo kwa sababu kila anapopata muda uonanan na mtoto wake ingawa  baba yake amekuwa hajui ilo..

ninaongea nae kila mara kwa simu, na pia nilishakwenda kumuona nyumbani zaidi ya mara tatu,sema tu baba yake na mtoto hajui hivyo labda kwa sababu pia hajawahi kumuuliza mama yake ninayemkuta nyumbani . Alisema Siwema .

Ney Wa Mitego Athibitisha Hakuna Ugomvi Kati ya Godzilla na Billnass

                                                     

 

Msanii wa bongo fleva anaetamba na kibao chake cha makuzi ney wa mitego amesema kuwa hakuna ugomvi wowote kati ya msanii Godzilla na Billnass kama watu wanavyosema katika mitandao, Ney wa Mitego amesema hayo baada ya kuwakutanisha wasanii hao wawili na kuweza kufanya nao kazi moja ambayo  inajulikana kama  muda wetu Remix ambayo pia ameshirikishwa AY.

Katika mitandao na baadhi ya vyombo vya habari kulikuwa na maneno kuwa billnass amekuwa akiiga nyayo za godzilla na kwamba kutokana na hayo wawili hao wamekuwa na bifu la kimuziki kutokana na maslahi ya musiki huo.

Akiongea katika Radio One , Nay wa Mitego amesema kuwa wsanii hao wawili hawana tofauti yoyote kama watu  wanavyosema kuwa wamekuwa na tofauti ya muda mrefu na kwamba nafasi ya Godzilla amezibwa na billnass katika game.

Mdundo ulinifanya nimuone Godzilla lakini pia mdundo ulinifanya nimuone  pia Billnass, licha ya kuwa kumekuwa na maneno katika mitando kuwa wili hao wamekuwa na tofauti ya muda mrefu lakini watu hao hawana tofauti yoyote.-Alifunguka Ney Wa Mitego.

Hata hivyo ney wa mitego aliongezea na kusema kuwa watu wengi katika mitandao wamekuwa na tabia ya kuvuruga maneno na kuzusha vitu vya uongo bila kujua ukweli wa kila kitu.

Naweza kusema kuwa mitandao au maneno ya watu yanaweza kuchochea kitu  na watu wakafanya kukawa na ugomvi, na ugomvi ukawa mkubwa wakati watu  wanakuwa hawana tofauti yoyote.-Alimazia Ney wa Mitego

 

 

Nay Wa Mitego Kumlipisha Diamond Fidia

Ikiwa bado anaendelea na kesi yake ya kutakiwa kulipa fidia kwa wasanii wakongwe nchini  wa band ya Msondo Ngoma baada ya kutumia ala yao ya sauti  Saxophone na kuweka katika wimbo wao wa Zilipendwa, hivi karibuni tena Diamond ametoa wimbo mpya ambao pia umekuwa na vionjo vya wimbo wa Ney wa Mitego unaojulikana kama makuzi ambao Diamond ametoa akimshirikisha msanii mkubwa Dunianai Rick Ross.

anaemiliki muziki huo wa makuzi ney wa mitego   anaweza kuwashitaki wasafi kwa kutumia kionjo hicho cha muziki wake bila kuwa na ruhusa yake.uongozi wa free nation ambapo ndio anapofanyia kazi ney wa mitego wana haki ya kudai fidia baada ya msanii huyo kutumia baadhi ya sehemu za wimbo wao katika wimbo mpya wa diamond.

Hata hivyo uongozi wa Free Nation chini ya Ney wa Mitego amesema kuwa wameamua kuwapa muda Wasafi na kujifikiria nini kufanya kabla  hawajaamua kuwapeleka mahakamani.

Hata hivyo meneja wa Diamond ,Babutale amejibu tuhuma hizo na  kusema kuwa wako tayari kukaa mezani na viongozi wa Free Nation ili kulizungumzia swala hilo hata hivyo meneja huyo alionekana kujiamini na kusema kuwa siku zote anaedaiwa huwa ni tajiri huwezi ukakuta maskini anadaiwa hata siku moja.

kumekuwa na malalamiko mengi kwa wasanii wa Tanzania kuibiwa baadhi ya maneno, mashairi au vionjo vya nyimbo zao bila kunufaika na nyiimbo hizo, Free nation hawatakuwa watu wa kwanza kutoa malalamiko , wapo wasanii wengi amabo wamekuwa na malalamiko ya aina hii.

Nay Wa Mitego na Duma Wameingia Kwenye Bifu Zito

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ney Wa Mitego na muigizaji wa Bongo movie Duma wamejikuta wakiwa katika pande mbili tofauti za shilingi baada ya kuingia kwenye bifu zito.

Bifu hili lilianzia kwenye mtandao wa kijamii huko Instagram baada ya Nay Wa Mitego kuweka maoni kwenye picha hiyo kulikuwa kuna wakali watatu wa Bongo movie ambao ni Rammy Gallis, Gabo na Duma na kisha ilisindikizwa na swali liliouliza ‘Je nani  mkali wa fasheni hapo?’ Basi baada ya kuona hivyo Nay Wa Mitego alienda ku-comment na kuandika ‘ Tafadhali msimfananishe Gabo na vitu vya kipuuzi’ maneno ambayo yalimkera sana Duma.

Baada ya maneno hayo kuenea mtandaoni Gabo alimwaga povu lake kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha televisheni cha East Africa;

Kwanza nilikuwa Nairobi nafanya project nikaona hizo comments watu tofauti tofauti wakanitumia mimi nikafurahi nikaona ni kitu kizuri ila naomba nimwambie Bwana Emanuel,  Ney Wa Mitego ameingia choo cha Kasilo kwa sababu ameshawahi kumtibua Niva, alishawahi kumtibua Yusuphu Mlela akatulia tu ila mimi ni namba chafu asione watu wamenyamaza ila mimi peke yake namtosha Ney Wa Mitego yaani mimi ndio namwambia Ney asiingilie mambo ya Bongo movie kama anatafuta kiki akatafute huko huko kwa wanamuziki wenzake asituingilie Bongo movie kwa sababu ameshatuongelea sana mara oh Bongo movie imekufa mara nini sijui sasa basi inatosha namkanya Ney aachane na sisi kama hana ishu arudi kwao Manzese akawe mkabaji maana alijuwa kibaka zamani hivyo awe na heshima maana mwisho wa siku mziki wake umeshuka”.

Pia Duma amedai Ney hana haki ya kuiongelea vibaya Bongo movie kwa sababu pale alipo hana kolabo hata moja na nsanii wa nje lakini hao anaowasema Bongo movie wameigiza na wasanii mbali mbali wa nchi za nje.

Ney Wa Mitego Amekuja Na nguvu Ya Kitaa

Msanii wa bongo fleva Ney wa Mitego amekuwa mbunifu na kuja na tour ya muziki inayojulikana kama nguvu ya kitaa ambayo itajikita kusabahi mashabiki wote waliopo kitaani, kwa sababu wanaami kuwa mtaani ndipo mashabiki wanaowapa viburi katika kazi wanapatikana.

Akiongea katika kipindi cha Siz wa kitaa cha Clouds Tv, msanii Ney wa Mitego alisema kuwa ziara hiyo inayojulikana kama nguvu ya kitaa imekuwa na lengo la kuwafikia mashabiki wote wanaopatikana mitaani tena hasa uko uchochoroni kwa sababu anachoamini yeye ni kuwa wanaosapoti na kupenda  muziki wao ni watu kutoka katika mitaa tu na wala sio  watu  matajiri kama watu wanavyofikiria

Tumeamua kurudisha fadhila kwa mashabiki wetu ambao wanapatikana mitaani, watoto wa mitaani kama tandale, masaki na sehemu za watu wa chini ndio wanaosapoti muziki wetu na wala sio watoto wa kishua, hata hivyo ukiangalia wasanii wengi wa muziki tumetokea huko kwenye maisha magumu wala sio maisha mazuri hivyo ni bora kuwa kumbuka wenzetu wa hali ya chini ambao wanatupa jeuri ya kuafnya kazi mjini

Hata hivyo akiendelea kuoingezea anasema kuwa shoo iyo itakuwa inagharimu kiasi kidogo cha shilingi elfu tatu tu kila sehemu na itaanza asubuhi ya saa nne mpaka pale watapoona mashabiki wao wametosheka na muziki wao.

Hata hivo, Ney wa Mitego anaendelea kusema kuwa katika mitaa yao kuna shida nyingi za kijamii hivyo fedha zitakazokuwa zinapatikana zitakuwa ni kwa ajili ya kusaidia sehemu hizo, kama hospitali na vituo vya watoto yatima na wafanyabiashara ndogondogo watakaokuwa wanakutana nao mitaani.Akitolea mfano anasema kuwa hata yeye alishaenda kwenye hospitali moja na kutoa kidogo alichokuwa nacho ili kusaidia hospitalini hapo.

Tamasha hilo ambalo limeanza jumamosi ya tarehe 04, katika viwanja vya Tanganyika Peakers linategemea kuendelea kwa baadhi ya mikoa ili kuwafikia mashabiki wanaopatikana katika mitaa na ambao hawaezi kwenda kwenye viwanja vya starehe kwa gharama kubwa ili kuwaona wasanii wao kwa bei ndogo.

Mziki Wa Bongo Fleva Unakufa Kwasababu Ya Wasanii Kupenda Kiki- Ney Wa Mitego

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Ney Wa Mitego amefunguka na kuamua kuwachana wanamuziki wenzake wote anaodai kuwa wanapenda kutafuta kiki kuliko kufanya mziki unaoeleweka.

Ney Wa Mitego alitumia mtandao wa kijamii kufikisha ujumbe wake ambao alidai wasanii wa bongo fleva kupenda kutafuta kiki kunapelekea kuua mziki kwani kiki inakuwa kubwa na mziki unakuwa wa kiwango cha chini sana kupita promo uliopata.

Ney Wa Mitego alifunguka:

Wasanii wenzangu kusema kweli kuna kitu nakiona kwenye gemu yetu, kwenye mziki wetu wa bongo fleva tuna kibarua kikubwa cha kurudisha mziki kwenye mstari ulionyooka kwa sababu imefika time watu sasa hivi wanatengeneza kiki kubwa alafu mziki mdogo, yaani kiki zimekuwa mbele mziki uko nyuma unasindikiza, tukiendelea hivi miaka miwili mitatu ijayo naiona bongo fleva ikiwa imepotea kama bongo movie ambavyo imepotea, Kama tusipokuwa makini kuamua kufanya kazi na mini viwe ni vitu vya kusindikiza mziki, sahivi mambo yamebadilika imefika time watu wanatengeneza kiki ambazo yaani hazielezeki alafu mziki unachukua nafasi ndogo sana unasindikiza kiki jamanii ehee tunajisahau tuamke turudishe mziki wetu kwa sababu tunakuwa tunawalemaza sana mashabiki zetu”.

Wasanii wengi wa Bongo fleva siku hizi wamekuwa na kawaida ya kutengeneza kitu kinachoitwa kiki yaani wanajitengenezea  skendo kubwa kwenye mitandao ya kijamii mara tu pale wanapokaribia kutoa nyimbo mpya ili tu wawe wanazungumziwa kipindi nyimbo inatoka kwa madai kazi inapata promo kubwa na ushabiki mkubwa.

 

 

Nay Wa Mitego: Nimeshazoea Kuishi Maisha ya Kimaskini

Mwanamuziki Wa Bongo fleva Ney Wa Mitego amefunguka kuwa ameshazoea kuishi maisha ya kimaskini kama Mtanzania yoyote yule mwenye kipato cha hali ya chini.

Ney alifunguka hayo baada ya habari kuenea kuwa ameuza nagari yake yote na anaonekana mtaani akitembea kwa miguu na kupanda bajaji, huku watu wengi wakidai kuwa amefulia ndio maana ameamua kuuza magari yake yote.

Katika mahojiano aliyoyafanya na kituo cha televisheni cha East Africa Ney alimwambia mwandishi anatamani Watanzania waache apumue na waache kumsakama kuwa amefulia kwani ndio maisha aliyoyachagua mwenyewe.

Ney alifunguka;

“Jamani niacheni nipunue haya ndio maisha yangu niliyoyachagua, kupanda daladala ama Bajaji ni sehemu ya maisha yangu, Mimi nimetokea mtaani siwezi kuishi bila kuheshimu mitaa, jata marafiki zangu ukiwaangalia ni Wa kawaida Sana, kwaiyo kutembea kwa miguu isiwe tabu, halafu Kama hujagundua mimi napenda maisha ya kawaida, siishi kistaa Kama wengine, na pia nikiishi hivi nakuwa huru zaidi”.

Ney Wa mitego amwyaongea hayo baada ya kuzidi kuandamwa na maneno ya watu wanaodai ameishiwa hana kitu baaada ya kuonekana mitaani akipanda Bajaji na kusemekana ameuza magari yake yote aliyokuwa anamiliki.

 

Ney Wa Mitego Afunguka Kuuza Magari Yake Yote

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Ney wa Mitego hivi karibuni amekuwa akionekana kuwa akitembea kwa miguu na kukatiza katika mitaa mbalimabli huku kukiwa na tetesi kuwa ameuza magari yake yote aliyokuwa akitumia kwa usafiri.Hata hivyo wapo baadhi ya mashabiki walioanza kusema kuwa inawezekana msanii huyo amefulia hivyo ameona njia sahihi kwa sasa kurudi kiuchumi ni kwa kuuza magari yake yote ili kuweza kujimudu katika swla la kipato.Baada ya kuzuka kwa maneno hayo  msanii huyo ameamua kufunguka na kuongelea swala hilo kiundani huku akikubali ni kweli kuwa ameuza magari yake yote lakini hakuweza kuweka wazi sababu zilizomfanya auze magari yake yote.

Akiongea na channel ya EATV, msanii Ney wa Mitego amesema kuwa”kila mtu anazungumza lake ujue,lakini kama kuuza nimeuza kwa sababu zangu binafsi za kimsingi.Nimeamua kuachana na magari na nimeamua kupanda daladala na bajaji na hayo ndo maisha yaNgu ambayo nilikulia, unajua mimi nimezaliwa katika maisha ya kawaida sana, na mtaaa ndo umenilea” alizungumza Ney wa Mitego.

Hata hivyo akiongezea kwa undani zaidi Ney wa Mitego anasema kuwa endapo atakuwa akionekana mitaani basi watu wasisiste kumpa lifti maana ndio maisha ya kusaiidiana,”watu waasichoke kunipa lifti wakiniona barabarani, au wasishangae wakiniona natembea kwa miguu” aliongezea Ney wa Mitego.

Hivyo basi kwa baadhi ya mashabiki ambao wamekuwa wakihofia labda msanii wao amefulia, basi waridhike na majibu ya msanii huyo kuwa kwa sasa ameamua arudi katika maisha yake ya kawaida ya mtaani na nadhani hii itakuwa njia sahihi zaidi kwa msanii huyu kuwa karibu na mashabiki wake kuliko ambavyo angekuwa akitumia gari lake.

Ney wa Mitego ni mmoja wa wasanii wanafanya vizuri katika nyimbo zake ambapo hivi karibuni ametoa vibao kama ‘Maku-zi’ ambao umekuwa ukifanya vizuri katika vituo mbalimbali vya Radio na Televisheni, lakini Ney wa Mitego  ni mmoja wa wasanii anaesifika kwa kusema ukweli juu ya kitu chochote kinachomkwaza bila kuogopa kitamlenga mtu gani.

 

Lulu Diva Amkana Ney Wa Mitego Hadharani.

Ni zaidi ya mwaka saa tangu kuwepo kwa habari kuwa msanii wa kike Lulu Diva kuwa na mahusiano na msanii anaefanya vizuri katika kazi zake za muziki Ney Wa Mitego, mwanadada huyo akanusha tuhuma hizo na kukutaa kata kata huku akisema kuwa Ney hana sifa za kuwa mpenzi wake.katika kipindi cha nyuma wawili hao walikuwa wakionekana pamoja na hata kuna baadhi ya mahojiano waliyokuwa awakifanya walikiri kuwa pamoja lakini cha ajabu ni kwamba kwa sasa mwanadada huyo amekataa kata kata kuwa yeye hana mahusiano na Ney Wa Mitego.

Hata hivyo Lulu Diva ameamua kutoa povu ili na kulielekeza kwa Ney Wa Mitego na kusahahu kuwa alishawahi kukiri kuwepo kwa uhusiano wao.’Ney hawezi kuwa type yangu hata siku moja,na hajawahi na hawezi kuja kuwahi  hata siku moja niwe na Ney” aliongea Lulu Diva

Hata hivyo Lulu aongezea kwa kusema kuwa Ney Wa Mitego hajawahi kumvutia kabisa katika swala zima la mapenzi.”kwanza hajawahi kunivutia, na kamwe hawezi kunivutia, hivi mimi kweli niwe na Ney, haiwezekani kabisa  kwa mwanaume kama yule” aliendelea kusema. Msanii huyo  wa kike ambae kwa hivi sasa na yeye ameamua kujishughukisha na shughuli za muziki kwa kuimba ilhali kipindi cha mwanza alikuwa ni video queen wa baadhi ya nyimbo za wasanii wenzie lakini pia ametokea katika baadhi ya tamthilia mbalimbali katika vituo vya televisheni.Amekuwa  akifanya vizuri katika kazi zake za muziki na  kutoa nyimbo kama ‘Usimwache’,’Utamu’ na ‘Give to me’ .

Ikiwa ni muda sasa umepita tangu wawili hao wafanye interview ikimuonyesha Lulu Diva akiwa na Ney Wa Mitego huku wakikiri kuwa walishawahi kuwa wapenzi lakini kwa sasa ni marafiki na kukiri wanaweza kufanya kazi pamoja kwa sasa muda wa mapenzi ulishakwisha na wakiamua kufanya serious basi wataweza kufanya muziki, inakuwa ni hali ya kushangaza kwa Lulu Diva kukataa kuwepo kwa mahusiano  baina ya wawili hao. hata hivo inawezekan akukawepo kwa marumbano baina ya wawili hao inayopelekea kuwepo kwa maneno hayo.

Salamu Za Wasanii Kutoka kwa Ney Wa Mitego

Akiwa ni mmoja kati ya wasanii wanaofanya vizuri katika tasnia hii ya muziki, mwanamuziki wa Bongo Fleva Emmanuel Elibariki  Ney Wa Mitego  “True Boy” ameamua kuwashauri wasanii wenzie wanaokaa kimya kwa muda mrefu  bila kutoa nyimbo huku wakitegemea kuwa watakapotoa  watapokelewa vizuri na mashabiki zao.

Ney wa mitego ameyaongea maneno hayo alipokuwa kwenye mahojiano  na kituo cha  Televisheni Cha Taifa ‘Tbc’ katika kipindi cha Papaso , Ney Wa Mitego  anasema kuwa kwa sasa game la muziki limebadilika  sana hivyo si vizuri kwa wasnii  kukaa kwa muda mrefu bila kutoa wimbo kama walikuwa wamezoa hapo mwanzo.

“huo muda umeisha, this time mtu akirudia hivyo basi tenaa!!yaani tunamsahahu kabisa, game hilo halipo tena”alisema Ney Wa Mitego.

Kwa muda  sasa   kumekuwa na tabia za mazoea  kwa   baadhi wasanii wa muziki  kukaa  kimya kwa muda mrefu sana  bila kutoa nyimbo  mpya wamekuwa  wakisahau kabisa  kuwa wanafanya baadhi ya mashabiki  wao kuwa na kiu na kuchoka kusubiri kwa muda mrefu, hata hivyo kutoa nyimbo kila baada ya muda pia kunafanya kukua kwa muziki.

Hata hivyo, katika maneno hayo aliyosema  Ney wa Mitego hakuonesha kumlenga msanii yoyote  ingawa ni kawaida kwa baadhi ya  wasanii wakubwa wa muziki kukaa kimya mpaka mashabiki zao wanaanza kurushiania maneno katika mitandao huku wakimuuliza anatoa lini nyimbo mpya. Kama msanii  alikiba ni mmoja wa wasanii wenye  tabia ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kutoa nyimbo, hivyo kama msanii   Ney Wa Mitego ametaka anajaribu kuwahasa wasanii wenye tabia hizo   kuacha  kwa sababu game la muziki  limebadilika watafikiri mashabiki wanawasubiri kumbe ndo wanawapoteza mashabiki.

Ney Wa Mitego ni moja kati ya wasani ambao nyimbo zao zinapendwa na mashabiki kwa sababu uongea ukweli katika mashairi yake bila kuogopa, mara nyingi amejikuta hata akiingia katika majibizano na baadhi ya wasanii wenzie kwa sababu ya kusema ukweli wao. Kwa sasa anatamba na kibao chake kinachokwenda kwa jina la “Makuzi’