Nuh Mziwanda afanyiwa upasuaji wa shingo

Msanii wa Bongo Nuh Mziwanda ameandika ujumbe kuwashukuru madaktari wa hospitali ya Mwananyala kwa kumfanyia upasuaji wa shingo baada ya kupata maumivu makali shingoni.

Nuh Mziwanda anayejulikana kwa hit song yake ya Jike Shupa, aliweka picha huku akionekana na bandage shingoni na tabasamu usoni kwa upasuaji salama.

Ingawa bado hajafunguka kusema kilichotokea, Nuh aliandika ujumbe kusema,

“Thanks Jesus….thanks MY SUPER DR KIWALE BINGWA kabisa wa upasuaji ‘Na MWANANYAMARA HOSPITAL kwa surgery (Upasuaji)uliokua chini ya shingo yangu’ bila kusahau MAMA yangu na ndugu zangu waliokua pamoja na mimi.naomba Maombi yenu Mashabiki wangu nirudi katika hali yangu na Kazi ziendelee.Love you.”