Paul Clement Amkana Emmanuel Mbasha

Msanii wa nyimbo za injili Emmanule Mbasha mara nyingi amekuwa akionekana katika baadhi ya post zake akisema kuwa yeye ndio mleiz wa wasanii wote wanaoimba injili nchini Tanzania na hata kuna baadhi ya mambo amekuwa akitaka kuyabebeba majukumu akiwa kama mlezi wa nyimbo za injili.

Swali linakuja je , wasanii wanajua kuwa yeye ndio lezi wao wa nyimbo za injili, jibu tunalipata kwa wasanii wenyewe kuhusu kiongozi wao huyo.

Mwanahabari Hassan Ngoma alipata fursa ya kuuliza swal hilo msanii paul clement alipokuwa katika mahojiano asubui ndani ya 360 ya clouds media, na mwanainjili huyo alikata na kusea kuwa kwa upande wake yeye kiongozi wake sio Emmanuel Mbasha bali ni mchungaji wake.

Paul anasema”Mmmh hapana , mimi mlezi wangu wa injili ni mchungaji wangu

Ben Pol Amenifundisha Muziki:-Paul Clement

Msanii wa muziki wa injili Paul Clement amefunguka na kusema kuwa hakuwahi kujua kama angeweza kufanya vizuri katika muziki ila kwa msaada wa msani wa bongo  fleva Ben Pol aliweza kufanikiwa katika muziki kwa sababu aliweza kumsaidia na kumfunidsha kuimba.

Paul Clement hakuona aibu alipokuwa akiongea na kipindi cha Pambio Live cha Kenya kuhusu kukua kwake kimuziki tangu anaanza kufanya muziki.

Ben Pol alinifundisha muziki,yeye ndio alinifundisha kuimba.Nilikuwa nikienda katika mashindano fulani kuimba nikawa nafukuzwa stageni na ninaambiwa kabisa toka haujui kuimba nenda kajifunze kuimba.Lakini Ben Pol alinifundisha kuimba na nilirudi palepale waliponiambia sijui kuimba nikaenda kuwaonyesha kwa sasa najua kuimba , nilitaka kuwaonyesha kuwa najua.Baada ya hapo nikaanza kuimba katika kundi moja la muziki wa injili la Glorious Celebration.

Sio kila msanii anaweza kuweka wazi kuhusu swala la yeye kufundishwa katika muziki tena hasa pale unapoiona kuwa status yako ni kubwa kwa mashabiki, wasaniiwengi wamekuwa waoga kukiri kuwa pale walipo kuna watu waliwahi kuwashika mkono nyuma yao.

Paul clement ni moja ya wasanii wakubwa wa injili wanaoimba kwa kutoa ujumbekatika jamii yake lakini pia amefanya muziki wake kuweza kupendwa  hata na nchi za jirani.

Paul Clement Asema, Makanisa Yanasaidia Muziki wa Injili Kuendelea

Msanii wa muziki wa injili nchini Paul Clement aliejulikana sana na kibao chake cha Amenifanyia amani , amefunguka na kusema kuwa kunakuwa na utofauti mkubwa sana kati ya muziki wa bongo fleva na ule wa injili kwa sababu katika muziki wa bongo fleva uzuri wa nyimbo zako ndio utakaokufanya uweze kupata show na kuuza jina lako lakini hii ni tofauti sana na mpango katika muziki wa injili.

Paul anasema kuwa katika muziki wa injili kuna wasanii hawajulikani kabisa katika jamii lakini ukienda huko makanisani wao ni wasanii wakubwa na kila siku wamekuwa wakitoa nyimbo impya na zinafanya vizuri, hibyo hii nitofauti sana na huko kwenye bongo fleva.

kwetu huku ni tofauti kidogo,kuna waimbaji wapo lakini huku katika jamii zetu za nje hawafahamiki kabisa,lakini lakini anakuwa anafahamika sana makanisani.yaani unakuta ni watu wakubwa sana na wanafanya kazi nzuri tu hii ni kwa sababu sisi tunapata bahati ya kuzunguka makanisa mengi sana, unakuta umezunguka dar makanisa karibiayote, mwanza makanisa yote .

sasa hii inawafanya wasanii wa injili kujulikana kila kona.makanisa yanasaidia sana wasanii wa injili na kuwafanya wasanii waendelee kuwepo hata kama umeleta wimbo wa aina gani, unakuweposehemu ya kupokelewa.

Msanii huyu anasema kuwa makanisa yanawafanya wasanii wengi wanaendelea kuwepo kwa sababu wanapata sehemu za kutambulisha nyimbo zao hata kama ni mbaya kwa sababu kanisani nafasi kama hizo zinakuwpo muda wote.