Queen Darleen Ajibu Tetesi Za Mama Yake Kufungwa China Kisa Madawa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na First Lady wa WCB Mwanahawa Abdul maarufu kama Queen Darlene amefunguka na kukana tetesi za mama yake kuwa kifungoni nchini China.

Miezi michache iliyopita kuna tetesi zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mama yake Mzazi na Queen Darlene amekamatwa nchini China Baada ya kukutwa na madawa ya kulevya na hivyo yupo jela akisota.

Katika mahojiano aliyofanya na Global Publishers juu ya ishu hiyo, Darleeen aliweka wazi kuwa, aliposikia hata yeye alishtuka na kwamba ni uvumi tu kwani mama’ke yupo hapa nchini na hapendi mambo ya mitandao.

Mama yangu kafungwa China? Niliposikia nilishangaa sana kwani mama yangu yupo na mtu akitaka anione nimpeleke nyumbani”.

Licha ya Queen Darlene kuwa na mama tofauti na msanii mwenzake na kaka yake Diamond Platnumz lakini Wana baba mmoja ambaye ni Mzee Abdul Juma.