Rick Ross Aongea Kitu Kuhusu Kufuta Picha za Diamond.

Siku chache zimepita tangu katika mitandao ya kijamii kuzizima baada ya kuonekana kwa akaunti ya msanii mkubwa nchi Rick Ross kufuta picha za msanii mkubwa kutoka Tanzania Diamond Platinumz ilhali wawili hao wote ni mabalozi wa kinywaji cha Belaire, kinywaji kikubwa na chenye bei ghali sana.

Maswali mengi yaliibuka kwanini msanii huyo alifuta picha zote za Diamond na kuacha za balozi wa kike Huddah Monroe.Lakini jibu limekuja kuatikana baada ya msanii huyo kuweka picha nyingine ya diamond na kuandika maneno ya kumsifia.Katika ukurasa wake wa instagram rick ross aliandika diamond is legend kumaanisha kumpa sifa .

Wataalam wa mambo wanasema kuwa inawzekana kufuta kwa picha za Diamond katika ukurasa wa instagram wake itakuwa ni maswala ya kibiashara au kuna sababu ya muhimu lakini sio kwamba wawili hao wanaugomvi au hawako vizuri.

Hata hivyo meneja wa Diamond Sallam _Sk alifunguka na kulizungumzia hilo na kusema kuwa huwa inatokea mtu anaweka picha na baadae anazifuta kwaio iyo pia imetokea hata kwa msanii mkubwa Dunianai Rick Ross kufuta picha hizo.

Ninavyofahamu wasanii wengi huweka picha za kusapoti au kuweka tangazo lakini ikifika muda huweza kufuta zile picha ,na hata diamond mwenyewe huwa nafuta zinapoisha muda.