Riyama Ally Ajitetea na Ubonge Wake

Msanii mkongwe wa filamu za Bongo movie, Riyama Ally ameibuka na kuwajia mashabiki zake ambao wamekuwa wakimtolea maneno kuhusu mwili Wake na kumtaka apungue.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Riyama  amewataka mashabiki wanaojitokeza na kumwambia apungue waache kufanya hivyo kwani anapenda alivyo:

https://www.instagram.com/p/BtgAqlvn62w/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1k4njqwbxukcn

https://www.instagram.com/p/BtfSFT-HilC/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1gzkeq2oe0v80

 

 

a wakimtolea maneno ya

“Mume Wangu Ameniingiza Kwenye Bongo Fleva”-Riyama Ally

Msanii mkongwe wa filamu za Bongo movie Riyama Ally amefunguka na kuwekan wazi kuwa mume wake ambaye ni msanii wa Bongo fleva Hajji Mwalimu maarufu kama Leo Mysterio ndiye aliyemuingiza kwenye ulimwengu wa Bongo fleva.

Siku za hivi karibuni sauti ya Riyama Ally imesikika katika moja ya nyimbo mpya za Leo Mysterio unaoitwa Wanaume wa Dar na mara moja Riyama ameweka bayana kuwa pamoja na kuwa hana kipaji cha kuimba lakini mumewe alivyomuomba ilibidi akubali.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Riyama amesema kuwa, yeye si muimbaji kivile lakini linapokuja suala la kumsapoti mume wake, haoni shida kujiingiza huko.

Sina kipaji cha kuimba, napenda sana kuigiza ila nitakuwa namsapoti mista wangu katika nyimbo zake kama vile kuingiza maneno kuntu”.

Lakini pia Riyama ameweka wazi kuwa wimbo huo umetungwa maalumu kwa ajili ya kuwakumbusha wanaume wasiopenda kufanya kazi na kukaa vijiweni kuinuka na kuacha kuchagua kazi wakati wanategemewa.

Kama ni kijana akisikiliza wimbo huo ambao nami nimeimba, atapata fursa ya kujifunza jambo”.

Wanaotaka Nishuke Watasubiri Sana :-Riyama Ally

Mwanadada Riyama Ally kutoka kwanda cha filamu nchi amaewapa pole sana wale wanaokaa na kumuomba mabaya kwamba hana muda mrefu sanaa yake na kipaji chake kitashuka na jina lake halitakuwepo tena katika tasnia ya filamu nchini,.

Riyama ambae amekuwa moja ya wasanii wa kike wenye kipaji cha hali ya juu na kupendwa sana na watu kwa sababu ya kazi zao anasema kuwa wapo watu wanamuombea kushuka kwa kipaji chake lakini yeye anaamini kuwa mungu anamuongoiza hivyo hakuna linaloweza kuharibika.

Kwa wale wanaosubiri kushuka kwangu watasubiri sana,  kwa sababu kushuka kwangu ni ngumu sana  sitashuka mpaka uzeeni nitakuwa bora zaidi.

Riyama pia amewataka wasanii wenzake kuwa wakweli kila mara hasa wanapokuwa wanaulizwa juu ya wale waliowashika mkono na kuwavuta mpaka kufikia pale walipo.

 

Riyama Ally Akimbilia Kwenye Muziki.

Msanii wa maigizo na vichekesho nchini , Riyama Ally amefunguka jinsi alivyofurahi kupewa heshima na wasanii wa kundi la ROSTAM kwa kuingiza kionjo katika wimbo huo ambacho kimefanya wimbo kunoga zaidi.

Mwanadada huyo anasema kuwa kwake ni heshima kubwa lakini pia amefurahi kuona wimbo umepokelewa vizuri hata kama sio wa kwake lakini ameweka mkono wake pale na imekuwa ikifanya vizuri.

akiongea katika kipindi cha papaso la burudani Riama anahadithia ilivyokuwa kabla ya wimbo kutoka ‘meneja wa ROSTAm alinipigia simu akaniambia kuwa kuna sauti inatakiwa kuigizwa kwenye wimbo na mimi ndio mhusika, nikafika studio nikaingiza kile kionjo chini ya usimamizi wa mume wangu  nashukuru sana kwa sababu wimbo umetoka na umependwa

Mwanadada huyo anaeonekna kuwa na Vipaji vingi amekuwa moja ya chachu za sanaa kwa kazi zake nzuri anazofanya zinazoendana na uhalisia.

Riyama Amsifia Mume Wake kwa Kuwa Mwaminifu.

Mwanadada Riyama Ally amezidi kumsifia mume wake mpenzi kwa kusema kuwa mwanaume huyo ni mwaminifu sana kiasi cha kwamba amekuwa katika ndoa yao kwa miaka minne sasa lakini hajawahi kuona wala kuhisi mwanaume wake akiwa na mchepuko wala kukutana na meseji za ajabu katika simu yake.

Riyama na Rey walifunga ndoa miaka kama minne iliyopita na ni moja ya ndoa za wasanii zilizodumu na kutokuwa na skendo katika mitandao ya kijamii kila siku kutokana na kuweka sana mambo yao chini ya kapeti.

niko na mume wangu mwaka wa nne sasa na wala hata siku moja sijawahi kuona meseji ya mwanamke katika siku yake hata ya kusingiziwa tu– Anasema Riyama.

Riyama- Wasanii Wasitegemee Sanaa Tu Kuingiza Kipato

Msanii mkongwe wa Bongo movie Riyama Ally amefunguka na kuweka wazi kuwa wasanii wanatakiwa watafute njia mbali mbali za kuingiza kipato na sio sanaa tu.

Riyama amefunguka hayo alipokuwa anaongelea biashara zake anazofanya nje ya sanaa ya Bongo Movie ambapo amedai kuwa sanaa inaingiza hela pia.

Riyama ambaye amekuwa akifanya vizuri na biashara yake ya kuuza t-shirt ameiambia Bongo 5 kuwa pale msanii anapoamua kufanya biashara haimaanishi kuwa sanaa anayofanya haimlipi.

Hapana sio kweli, mtu unatakiwa kufanya vitu mbali mbali ili kuweza kujiongezea kipato lakini movie na tamthilia zinalipa na uzuri tunapiga miguu yote, basi mambo mazuri hiyo nimejiongeza tu“.

Imekuwa jambo la kawaida sasa kwa mastaa mbali mbali kufanya biashara hasa kwa kutumia mitandao ya kijamii kujipatia kipato aidha kwa kutangaza matangazo ya biashara au hata kuwa na biashara zao binafsi na kuzinadi kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Monalisa Afungukia Bifu La Wema na Riyama

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Ivyonne Cherry maarufu kama Monalisa amefunguka na kuongelea bifu lililosemekana lili kuwepo kati ya waigizaji wawili wa Bongo movie ambao ni Wema Sepetu na Riyama Ally.

Wiki chache zilizopita Wema alichukua tuzo ya Muigizaji bora wa kike kwenye Bongo movie Kupitia Tuzo za SZIFF ambayo alishindanishwa na wasanii wengi kama Riyama.

Baada ya Riyama kukosa tuzo ile alifanya Interview na kituo kimoja cha redio na alimwaga machozi live  kabisa huku akidai kuwa yeye alistahili kupata tuzo ile na kuwataka SZIFF wamuombe radhi kwani kukosa kwake tuzo ni Kumdhalilisha.

Baada ya kuongea maneno hayo moja kwa moja ilivhukuliwa kuwa Riyama amejijengea bifu na Wema Sepetu kwani ni sawa na alisema kuwa Wema hakustahili kupata tuzo hiyo.

Lakini Riyama na Wema walizima tetesi hizo za kuwa na bifu baada ya kupiga picha pamoja wakiwa Airport walipoenda kumpokea Monalisa ambaye alikuwa ametoka kuchukua tuzo yake nchini Ghana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Times Fm Monalisa alifunguka haya kuhusiana na maneno yaliyosemwa kati ya Wena na Riyama:

Kwanza niseme nilivyofika pale sikutegemea kuona watu lakini nilivyoshuka nikakutana na wasanii wenzangu, nilijisikia furaha sana..

Nilifurahi kuawaona, sidhani kama Riyama kamlalamikia Wema nyie tu ndio mnachukulia vibaya, Riyama alikuwa na malalamiko yake na mimi ninayafahamu toka siku ya kwanza”.

 

“Tuolewe na Wazee Watufie?” Riyama na Uwoya Kuhusu Kuolewa na Viben- 10

Muigizaji wa Bongo movie Riyama Ally amefunguka kuhusu kuolewa na mwanaume ambaye ni mdogo kwake kiumri ambapo amesema haoni tatizo na pia kuhusu Irene Uwoya kuolewa na Dogo Janja amesema ndio vizuri waolewe na wazee wawafie?.

Riyama Ally ameolewa na Mwanamuziki wa Bongo fleva anayejulikana kama Leo Mysterio ambaye kiukweli kabisa ni kiben10 kwake kwani ana umri mdogo kuliko yeye jambo ambalo Riyama amesema ndio anapenda hapendi wazee.

Riyama na Mume wake

Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni na Millard Ayo Tv, Riyama amefunguka na kusema kwamba haoni tatizo kuwa na mwanaume mdogo na hata alipoulizwa kuhusu rafiki yake Irene Uwoya kuolewa na kiben-10 Dogo Janja amedai ndio vizuri kutafuta kijana.

Irene Uwoya na Mume wake Dogo Janja

Kwenye mahojiano hayo Riyama alisema mambo haya:

Mimi nimempa ushauri Irene kama dada yake na rafiki yake nikamwambia kaza hapo hapo kwenye ndoa yako usilegeze maneno yatasemwa sana kama mimi ninavyosemwa kuolewa na Mume wangu niliyemzidi umri kwa sababu mapenzi furaha bwana kama furaha yako ipo hapo basi inatosha kwanini tukatafute wazee waje watufie ndani?”.