Mange Kimambi Amtolea Uvivu Roma, ni Baada ya Kufungiwa na BASATA.

Mwanaharakati Mange Kimambi amefunguka na kuelezea jinsi alivyoipokea hukumu ya Roma kutoka kwa Naibu Waziri wa sanaa baada ya kuonekana kuwa nyimbo ya msanii huyo  inayojulikana kama kibamia kushindwa kuiboresha nyimbo hiyo na kukaidi agizo za kuondoa baadhi ya maneno.
Mange Kimambi ambae anasema kuwa hakutaa kulizungumzia swala hilo lakini mashabiki wamemuhamasisha kuongea hivyo kwaio ataongea kama vile lilivyo katika uhalisia.

                                                

Mange Kimambi anasema kuwa Roma alikuwa muoga sana katika kumtetea Mbunge Sugu ambae aliwekwa gerezani kwa shughuli za kisiasa ingawa alikuwa na bado  ni msanii mwenzao, Mange anasema kuwa Sugu ni moja ya wasanii jasiri waliweza kusimama bungeni na kutetea muziki wa hip-hop Tanzania,lakini pia Mange Kimambi anasema kuwa hawezi kumtetea Roma kwa hilo kwa sababu kipind yeye anatekwa Sugu alikuwa mstari wa mbele kumtetea Bungeni na kuhakikisha kuwa swala la kupotea kwake linashugulikiwa lakini cha ajabu Roma hakuwahi kufanya lolote pale Sugu alipokamatwa.

I think ni bora wasanii wanyooshwe ili wapate hasira.roma kumtetea sugu tu ni mpaka tumchambe kwanza  na sio kumtetea tu lakini pia hata kumpost ilikuwa anaandika caption as if  n mtu kavunja  sheria  akafungwa kawaida.yaani kama vile ambavyo watu walikuwa wakimpost kajala na lulu walipoenda jela..kama yeye kaamua kuwa muoga basi na sisi ni lazima tuwe waoga kumtetea yeye.mbona sisi tulimtetea yeye kwani hatukuwa na watoto na wajawazito, kwani sisi hatuwazi kufa na kuziachaje familia zetu?roma hata kwenye kesi ya sugu hakutokea, apambane mwenyewe.-Alifunguka Mange Kimambi.