Mimi na Zari Hatuna Ugomvi;-Sallam K

Moja yamabosi wa msanii Diamond pPlatinumz,  Sallam k amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwamba hakuna mahusiano mazuri kati ya msani wake diamond na mama  wa watoto wake  lakini kwa upande wake na mwanamama huyo mahusiano yao ni mazuri na hakuna ugomvi wowowte.

Sallam anasema kuwa pamoja na yote lakini Zari na yeye wamekuwa wakiwasliana hata kuambiana maswala ya kibiashara na kama kuna ushauri wamekuwa wakipeana hivyo kwa upande wao hakuna shida yoyote.

mimi na zari hatuna tofauti yoyote, mpaka tunawasiliana na kupeana madili ya kibiashara na kama kuna ushauri anataka ninampatia.

Ikumbukwe kuwa Zari na Diamond wameachana kwa muda mrefu lakini wau wa karibu na msanii huyo wamekuwa wakiendelea kuwa na mahusiano nae pamoja na migogoro yote iliyopo kati ya wazazi hao.