“Mwambieni Uchebe Mwanamke Hachungwi” Dogo Janja

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri kunako tasnia hiyo Dogo Janja amempa ushauri mwanaume mwenzie Uchebe ambaye ameingia kwenye ndoa hivi karibuni ambapo amemfungukia na kumuasa kutomchunga mkewe Shishi.

Ikiwa miezi michache tu imepita tangu ndoa iliyofunga mwaka ifungwe kati ya Irene Uwoya na Dogo Janja ndoa iliyoongelewa sana na ndoa iliyofungwa kwa usiri Mkubwa sana.

Pamoja na ndoa ilikuwa ya siri na maisha yao yamekuwa ya siri sana mbali na mitandao ya kijamii lakini juzi kwenye harusi ya Shilole na Uchebe wawili hawa wameonekana hadharani kwa mara ya kwanza.

Kwenye sherehe hiyo ya ndoa ya Uchebe na Shilole ilihudhuriwa na mastaa kibao lakini Uwoya na Dogo Janja wanaweza wakawa wana mfanano mkubwa Sana na maharusi kwani wote walipitia vikwazo mpaka kufunga ndoa lakini pia walifanya ndoa za siri siri Sana.

Kwenye sherehe hiyo Dogo Janja alipiga stori na Dizzim Online na alikuwa na ushauri mmoja tu kwa Uchebe nao ulikuwa Mwanamke hachungwi:

Kiukweli harusi yangu ilikuwa ina privacy sana ila nahisi na sisi soon tutafanya kitu kama hiki tutashiriki na ndugu na marafiki lakini kikubwa nataka niwapongeze Shilole na Uchebe na ushauri wangu endapo yanatokea mambo ya kazi asimbane ampe nafasi kamkuta na kazi zake aendelee kuheshimu kazi za mwenzake na Shilole hivyo hivyo panini ninachomwambia Uchebe mwanamke achungwi sana mwanamke hachungwi kwanza unaanzaje kumchunga mwanamke”.

 

Tazama Mastaa Kama Diamond, Jux, Vanessa na Harmonize Walivyomwaga Mapesa Kwenye Harusi Ya Shilole

Usiku wa Jana ilikuwa sherehe ya harusi (Wedding reception) ya Shilole na Uchebe ambayo ilipambwa kwa kuhudhuriwa na mastaa kibao ambao walimwaga mapesa kwa maharusi.

Ingawa noa rasmi ilifungwa ghafla na kimya kimya mwaka Jana mwishoni kwenye harusi iliyohudhuriwa na watu wasiopungua kumi huku ndufu wa Shilole wakifanya fujo kwa kukataa harusi hiyo isifungwe ingawa mwishowe ikafungwa.

Siku ya Jana kwenye sherehe iliyofanyika rasmi ilihudhuriwa na mastaa wa Bongo movie na bongo fleva kama vile Irene Uwoya na Dogo Janja, Queen Darlene, Diamond, Jacqueline Wolper, Harmonize na Sarah, Babu Tale, Madee, Mbosso, Rachel kizunguzungu na wengine wengi.

Kama kawaida mastaa hao kila mmoja alipata wasaa wa kutoa zawadi kwa maharusi na walifanya kufuru kweli.

1. Harmonize na Sarah

Harmonize na mpenzi wake walianza kwanza kuwamwagua maharusi mahela kibao yaani kuwatunza na walifuatia kwa kuwazawadia gari aina ya Noah lenye thamani ya shilingi milioni Tisa za kitanzania.

2. Vanessa Mdee

Vanessa aliwazadia maharusi Shilole na Uchebe kiasi cha pesa ambacho kitatumika kugharamia honeymoon ambayo watakwenda baada ya ndoa.

3. Juma Jux

Msanii Jux aliwapa maharusi zawadi ya kumsomesha mtoto mmoja wa Shilole shule mpaka atakapomaliza masomo yake.

4. Diamond Platnumz

Kama kawaida ya Diamond alimwambia Shilole achague zawadi yoyote atakayotaka na yeye bilashaka atagharamia kwa pesaa yake mwenyewe.

 

 

Uchebe- Mimi Ndio Nimembadilisha Shilole Hasa Kwenye Suala la Kunywa Pombe

Uchebe ambaye ni mume wa mwanamuziki wa Bongo fleva Shilole, amefunguka na kudai kuwa ndoa yake kwa Shilole imembadilisha sana hasa kwenye suala la kunywa pombe.

Shilole na Uchebe walifunga ndoa ya siri iliyowashtua watu wengi mwezi mmoja uliopita harusi iliyohudhuriwa na watu kumi tu huku ndugu wa karibu wakipinga harusi hiyo kufanyika hadi kufikua hatua ya kupelekana polisi na dada yake kwa kile kilichodaiwa kuwa alifanya fujo ili kuzuia ndoa hiyo.

Lakini Shilole alisisitiza kuwa anampenda Uchebe na kuishia kufunga naye ndoa. Mwezi mmoja baada ya kufunga ndoa na Shilole, Uchebe amefunguka kuhusu maisha ya ndoa na mkewe.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ago Tv, Uchebe alizidi kufunguka yafuatayo:.

Tarehe ishirini inshallah mwenyezi Mungu akijaalia ndio tutafanya sherehe ya harusi yetu itakayo hudhuriwa na watu wengi zaidi ambao wanatutakia Kheri kea kweli. Lakini pia nashukru tangia tumefunga ndoa mke wangu kabadilika sana hasa suala la pombe kapunguza kabisa yaani hakuwa hivi kwa jinsi nilivyomkuta na sasa tofauti kabisa hata nyie watu mnaomjua mtaona kuna utofauti fulani ila pombe taratibu taratibu ataacha kabisa maana zamani ilikuwa unakuta mtu kaamka asubuhi kashalewa analewa siku nzima Lakini tangu tumefunga ndoa pombe anakunywa kidogo jioni mpaka jioni “.

Lakini pia Uchebe aneongelea suala la akaunti feki kwenye mitandao ya kijamii ambayo inatumia jina lake na kutukana watu ovyo na kuwasihi watu waipuuzie kwani ni wazi kabisa kuwa siyo yeye.

 

Shilole Amtolea Povu Mange Baada Ya Kumponda Uchebe

Mwanamuziki wa Bongo fleva Zuwena Ashraf ‘Shilole’ amemjia juu mwanaharakati wa siasa mtandaoni Mange Kimambi baada ya kumponda mume wake Uchebe.

Shilole alifunga ndoa na Uchebe wiki chache zilizopita ambayo ilikuwa ni ndoa ya kimya kimya au ndoa ya siri ilyohudhuriwa na watu wachache lakini iliyozua gumzo kwa sababu ya ugomvi wa familia iliyozua. Lakini tangu ndoa hiyo imefungwa Shilole amekuww na kazi ya kumtetea Uchebe endapo mtu yeyote atamponda.

Siku chache zilizopita Shilole alimtetea tena Uchebe baada ya Mange Kimambi kumponda Uchebe na kudai kuwa ana jina la kienyeji na mbaya. Baada ya kuona hivyo Shilole kupitia ukurasa wake wa Instagram alimwaga povu hili dhidi ya Mange:

Mange my sis nakuheshimu sana pliiiz mume wangu Uchebe mbaya pliiz muache mimi mdogo wako ndio nimeshampenda by the way nina safari ya kuja American soon”.

Lakini baada ya povu hilo Mange alimjibu Shilole kwa kumtaka radhi kumwambia alikuwa anamtania tu aliposema mume wake Uchebe ni mbaya na ana jina la kienyeji ambapo kupitua ukurasa wake wa Instagram aliandika:

I was just joking nakutakia kila la Kheri kwenye ndoa yako ukija kwa Trump basi uje na LA ila use umenisamehe kweli nisije nikaja nikajileta mtegoni alafu nikachezea kipigo cha mwizi maana hiyo sentensi nina safari ya kuja kwa Trump Ina maana nyingi alafu Uchebe shemela nilikuwa nakutania tu mimi mwenyewe jina langu la kienyeji”.

 

 

 

Shilole: Sijaingia Kwenye Ndoa Kwa Ajili Ya Kucheza Mduara

Mwanamuziki wa Bongo fleva Zuwena Ashraf ‘Shilole’ amefunguka na kudai hajaingia kwenye ndoa kucheza mduara yupo kwenye ndoa mazima.

Shilole alizua gumzo wiki iliyopita baada ya kufunga ndoa ya siri na kimya kimya pamoja na mpenzi wake ambaye kwa sasa ni mumewe Uchebe. Ndoa hiyo imezua gumzo Sana kwani ndugu wa Shilole hawakutaka aolewe na Uchebe hadi kufikia hatua ya Shilole kumpeleka Dada yake polisi baada ya kuchukua Simu yake ilimradi tu wazuie harusi hiyo.

Pamoja na misukosuko hiyo Shilole na Uchebe walifunga ndoa ambayo ilihudhuriwa na watu kumi tu. Lakini tangu ndoa hiyo imefungwa Shilole amekuwa mtu wa kulalamika maneno ya kejeli yanayorushwa na watu dhidi ya ndoa yake na Uchebe.

Shilole amefunguka na kusema kuwa watu wasimfikirie ameamua kuingia kwenye ndoa kama maonyesho bali amedhamiria kwenda  kuwa mke mwema anayestahili na kuwa mfano wa kuigwa.

Shilole ameongeza kuwa anajua wazi kuwa kuna watu wanamhesabia siku za ndoa yake kuvunjika kama ilivyo kwa mastaa wengine, lakini kwa jinsi alivyodhamiria kutulia kwenye ndoa yake atawashangaza walimwengu.

Najua wazi watu watakuwa wananihesabia siku ndani ya ndoa yangu lakini ukweli ni kwamba nitawashangaza watu wengi na sina sababu ya kuacha kuwa mke bora na mwenye heshima kwa mume wangu kipenzi Uchebe na uhakika Mwenyezi Mungu atatupa miaka mingi”.

.

 

Shilole Awajia Juu Watu Wanaoiponda Ndoa Yake na Uchebe

Msanii wa Bongo movie Zuwena Ashraf ‘Shilole’ amewajia juu watu wote walio kifua mbele kuisema na kuiponda ndoa yake na Uchebe.

Shilole na Uchebe walifunga ndoa ya siri wiki iliyopita iliyofanyika Nyumbani kwa Meneja wa Diamond Babu Tale na kugudhuriwa na watu wasiopungua kumi.

Tangu ndoa hiyo imefungwa kuna maneno mengi yameibuka mitandaoni hasa kwa sababu kuna ripoti zilizodai kuwa familia ya Shilole haikukubaliana na ndoa hiyo hadi kufikia hatua ya ugomvi mkubwa kutokea kati ya Shilole na Dada yake hadi kufikia hatua ya kupelekana polisi.

Baada ya maneno kuzagaa mtandaoni kuhusu Ndoa hiyo Shilole ameibuka na kudai kusikitishwa na habari za majungu zinazoendelea kusambaa kumhusu mume wake Uchebe:

Kwenye mahojiano na gazeti la Mtanzania Shilole amezidi kufunguka haya:

Mfa maji haishi kutapa tapa , Ndoa yangu imewaumiza wengi wasionipenda, nimeona maneno mengi ya kashfa na majungu wakinichafua sasa mimi nasonga mbele na maisha yangu sina habari na mtu”.

Lakini pia Shilole ameeleza kuwa pamoja na kwamba watu wanamchafua lakini anaamini ndoa yake itadumu na kwa sasa familia yake ipo vizuri na ndoa yake.

Shilole- Dada Yangu Hakutaka Niolewe Sijui Alijua Mimi Bikra?

Mwanamuziki wa Bongo fleva Zuwena Ashraf maarufu kama  ‘Shilole’ amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusiana na ndoa yake iliyofungwa wiki iliyopita.

Shilole na mume wake Uchebe walifunga ndoa ya kushtukiza na ya ghafla mapema wiki iliyopita. Ndoa hiyo ilifungwa kimya kimya huku ikihudhuriwa na watu wasiopungua ishirini.

Habari zilizotapakaa mtandaoni ni kuwa ndoa hiyo ilikuwa ya siri kwa sababu ndugu wa Shilole hawakutaka aolewe na Uchebe kwa sababu zisizojulikana na hivyo kupelekea wao kuisusia ndoa hiyo lakini pia kuna habari zilizodai kuwa Ndoa hiyo ilikuwa ya ghafla kwa sababu Shilole ni mjamzito.

Kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv Shilole aliulizwa hasa kwa nini ndoa hiyo ilikuwa ya ghafla na kwa nini ndugu hawakuhudhuria:

Ndoa ilikuwa ya kimya kimya kwa sababu walinifata Maustadhi wakaniambia ndoa haitangazwi inatakiwa kufanywa kwa siri kwa sababu husda nyingi na mambo ni mengi kwaiyo nikafunga Ndola ya kislaamu kwaiyo kilichobaki ni sherehe tu lakini kabla ya Ndoa kuna matatizo ya kifamilia tu yalitokea kuna Dada yangu hakutaka mimi niolewe lakini nilimwambia mimi nimeshafikia umri wa kuolewa sasa sijui ananionaga mimi bado bikra? Nikamwambia dada mimi nataka kuolewa nimeshapata mtu ninampenda usinichagulie mtu wa kuwa naye isitoshe bwana kanipenda nina watoto wawili tayari basi nikawa nishaamua mtu mwingine hawezi kunichagulia mwanaume”.

Shilole amesisitiza kuwa lengo lao la kufanya bonge la sherehe liko pale pale kwani tarehe ishirini na tano watafanya bonge la party watu watakula na kusaza mpaka watabeba takeaway.

Uchebe: Bora Kufa Kuliko Kumkosa Shilole

Uchebe Ashraf ambaye ni mchumba wa Mwanamuziki wa Bongo fleva, Shilole Kiuno amefunguka na kudai ni bora afe kuliko kuishi maisha yake bila kuwa na mpenzi wake Shilole.

Wiki iliyopita kuna habari zilienea na zikisindikizwa na picha iliyomuonyesha Shilole na mpenzi wake wa zamani Nuhu Mziwanda wakiwa kitandani wamelala kimahaba kabisa huku habari zikidai kuwa Shilole kamwaga mchumba ake Uchebe na kumrudia Nuh Mziwanda.

Lakini mara tu habari hizo zilivyoanza kuenea Shilole alitumia mitandao ya kijamii kukana taarifa hizo na kuweka wazi kuwa ile picha iliyokuwa inasambaa mtandaoni ilikuwa ni picha ya zamani enzi yupo na Nuh na aliyesambaza picha hizo ni Nuh katika jitihada zake za kutaka kumgombanisha na Uchebe, tuhuma ambazo Nuh alizikataa kupita kiasi.

Baada ya sakata hilo Mpenzi wa Shilole, Uchebe aliweka wazi kuwa taarifa hizo zilikuwa za kweli lakini pamoja na hayo kuliko kumuacha Shilole basi bora afe tu. Kwenye mahojiano aliyofanya na Over The Weekiend Uchebe amekiri kuwa pamoja na kuwa amegundua kuwa Shilole alirudisha penzi lake kwa bwana ake wa zamani Nuh Mziwanda lakini hayuko tayari kumuacha:

Najua Shilole amenikosea sana  lakini siko radhi kumuacha ninampenda mno na niko radhi kupoteza maisha yangu  kwa ajili yake au niuze chochote nilichonacho ilimradi tu nimridhishe kwa chochote atakacho yeye”.

 

 

Shilole Amtolea Povu Nuh Mziwanda na Kudai Anataka Kumgombanisha na Mpenzi Wake

Mwanamuziki wa Bongo fleva Shilole amemjia juu aliyekuwa mpenzi wake Nuhu Mziwanda na kudai kuwa anataka kumuharibia uhusiano wake na mpenzi wake Uchebe.

Siku ya Jana habari zilienea kuwa Shilole amerudiana na Nuhu Mziwanda na kumuacha mpenzi wake Uchebe. Siku chache zilizopita Uchebe na Shilole walitangaza kuwa wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na kudai kuwa wanataka kufunga ndoa yao Ulaya. Pia Shilole alimpeleka Uchebe Nyumbani kwao Tabora, Igunga ili kumtambulisha kwa wazazi wao.

Hivyo Jana baada ya habari kusambaa kuwa Shilole kamuacha Uchebe na kurudiana na Nuh Mziwanda watu wengi walishangaa kwani ni juzi tu habari zilisambaa kuwa Nuh Mziwanda amerudiana na make wake Nawal ili wamlee mtoti wao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Shilole amekataa vikali tetesi hizo za yeye kuachana na Uchebe na kurudiana na Nuh Mziwanda na hata kumnyooshea kidole Nuh na kudai kuwa yeye ndiye aliyesambaza habari hizo za uongo na ile picha ili mradi tu amgombanishe na mpenzi wake Uchebe.

Shilole ametoa tamko lifuatalo kutokana na tetesi hizo:

Ulizani utanikomoa kwa taarifa yako hiyo picha sio ya leo unaunga unga matukio ili kunigombanisha na mchumba wangu? Mashabiki zangu niwaambie tu hiyo staili ya nywele nadhani mnajua kuwa napenda kuitumia. Alipangalo Mwenyezi Mungu binadamu hawezi kulipangua”.