Uchebe Apongezwa Kwa Kumuachisha Pombe Shilole

Mume wa Msanii wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole, Ashraf Uchebe amepewa pongezi nyingi na wasanii mbali mbai Baada ya kuweza kumbadilisha mke wake.

Wasanii wa Bongo movie kama vile Jacob Steven ‘JB’, Steven Mengele ‘Nyerere’ na Single Mtambalike ‘Richie’ wamejikuta wakimpa ­pongeza shemeji yao, Uchebe kwa kumbadili na kumuweka kwenye maadili ya kidini tofauti na alivy­okuwa zamani.

Global Publishers wanaripoti kuwa tukio hilo la kumpongeza Uchebe lilichukua nafasi kwenye msiba wa msanii mwenzao Salome Nonge ‘Mama Abdul’ baada ya Shilole kuonekana kubadilika sana kwani hata mmoja wa wasanii alipommwagia pombe kwa bahati mbaya, alionesha kumaindi kuliko maelezo.

Jamani Uchebe hongera sana maana kazi uliyofanya sio ndogo, nakuambia ni kazi kubwa. Yaani dada yetu Shilole leo hii anaona pombe anaruka hivi? Shemeji yetu hongera, umetukosha“.

Shilole alifunga ndoa na Uchebe mwaka juzi na tangu afunge ndoa ameonekana akiwa kama mwanamke tofauti kama alivyokuwa awali na hata kuonekana akiwa ameanika dini zaidi.

Shilole Awatolea Uvivu Wanaommendea Uchebe

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amewajia juu na kuwatolea uvivu wanawake wanaomuwinda Mume Wake wa ndoa Uchebe.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shilole amevunja ukimya, awatolea uvivu wanawake wanaomuwinda mume wake akisisitiza ametumia nguvu kubwa kumpa mwonekano alionao sasa.

Niliridhika na hali yako tangu mwanzo Mpaka sasa unashaini ila wadangaji msivyo na haya mnaanza kumwambia mume Wangu Uchebe amekuwa handsome. Mkome namtunza zamani mlikuwa wapi?”.

Shilole alifunga ndoa na Uchebe Desemba ya mwaka 2017 kabla ya hapo Uchebe alikuwa Fundi gereji na asiyejulikana Lakini tangu ameanza mapenzi na Shilole ameonekana kunawiri na Hivi sasa anaishi maisha ya kifahari na msanii huyo.

Shilole Afungukia Mipango Ya Kuzaa na Uchebe

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka na kuwajibu watu ambao wamekuwa wakimteta kwa kuchelewa kwake kumzalia mtoto mumewe Uchebe waliyefunga ndoa mwaka jana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Dimba, Shilole amefunguka kuwa kushika ujauzito na kujifungua salama ni mipango ya Mwenyezi Mungu, hivyo hana haraka na hilo, kwani anaamini ni muda tu haujafika. ya Mwenyezi Mungu, hivyo hana haraka na hilo, kwani anaamini ni muda tu haujafika.

Nadhani kila kitu ni mipango ya Mungu, wakati ukifika kila kitu kitakuwa hadharani, kwani mimba ni pembe la ng’ombe halifichiki, alisema, Shilole“.

Shilole ameweka wazi kuwa kwa Hivi sasa yuko bize na shughuli zake za ujasiriamali, lakini wakati huo huo akiwa anaihudumia familia yake kama ilivyo kwa wanawake wengine.

Shilole Afungukia Sababu Za Kutomzalia Uchebe

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Zuwena Mohamed maarufu Kama Shilole amefunguka na kuanika sababu zinazomfabya mpaka leo hii asimzalie mume Wake Ashraf Uchebe.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Enews cha EATV, Shilole ameweka wazi kuwa sababu pekee iliyomfanya Mpaka sasa hajamzalia Mumewe Uchebe ni sababu anaamini Mungu bado hajambariki Mtoto kwa sasa kwani Mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu.

Lakini pia Shilole ameweka wazi kuwa wao Kama wana ndoa wamekuwa wakijaribu kwa kipindi kirefu sasa kutafuta Mtoto lakini majaaliwa ya Mwenyezi Mungu hayajatimia bado.

Sisi tulikuwa tunatafuta Tupate Mtoto lakini bado hatujajaliwa, unajua mtoto sio kwamba mtu unapachikwa tu, mtoto anatafutwa na hatafutwi siku moja watu wanakaa miaka hata 10 na hwapati Mtoto na wako kwenye ndoa, Mimi tayari Nina watoto wawili na hata hao wengine hawakupatikana hivi hivi”.

Shilole tayari ni mama wa watoto wawili wa kike aliozaa na aliyekuwa mume Wake ambaye pia alifariki Wiki chache zilizopita.

Shilole Afungukia Mkosi Wa Nyumba Yake Mpya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka na kuweka wazi kuwa baada ya kuhamia kwenye mjengo wake mpya lakini amekiri kukaribishwa na mkosi.

Global Publishers wanaripoti kuwa Shilole alitokelezea kwenye uzinduzi wa Albamu ya Nandy lakini Ghafla aliibua minong’ono Baada ya kuonekana na nundu usoni hali iiyopelekea watu kudhani huenda Mumewe Uchebe amemtembezea kichapo.

Katika mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda Shilole alifunguka na kusema:

Aaa…Unajua juzijuzi ndiyo nimehamia nyumbani kwangu Majohe, sasa nyumba yenyewe bado sijaizoea na bado sijaweka umeme, sasa niliporudi usiku nikiwa nimechoka ndiyo nikajikuta napiga mwereka na kuumia hivi.

Si unajua nyumba usiyoizoea? Hayo ndiyo yaliyonikuta na hii pati kwa kuwa nilishaalikwa na kumhakikishia Nandy kuwa nitakuwepo, nimeona nijikongoje nifike haina jinsi”.

Miezi michache iliyopita Shilole alianika mjengo Wake mpya alioujenga kwa kutumia pesa aliyopata kupitia Sanaa na biashara zake.

 

Shilole- Wivu Ndio Umempelekea Uchebe Kuwa Video King

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka na kuweka wazi kuwa sababu za mume wake Asharaf Uchebe kuwa video king kwenye video yake.

Siku chache zilizopita Shilole ameachia wimbo wake mpya unaoenda kwa jina la ‘Champion’ na ndani ya video hiyo mumen wake Uchebe amesimama kama video king hali iliyopelekea mashabiki kuhisi huenda msanii huyo amejiingiza kwenye sanaa rasmi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers , Shilole alisema kuwa, mumewe huyo huwa hapendi sana kumuona akishuti video na wanaume huku ‘akibambiwabambiwa’ hivyo ili kumfanya awe na amani ndipo akamtumia yeye kwenye video hiyo.

Ule wimbo kwanza nilimuimbia yeye, lakini Uchebe ana wivu sana, huwa hapendi kuona nashikwashikwa na wanaume kwenye video au hata kwenye steji, ndiyo maana nikaona kwa wimbo huu ambao nimemuimbia, siyo vibaya nikamtumia na kakinogesha kichupa ile mbaya”.

 

Uchebe Atangaza Vita Kwa Wanaume Wanaommendea Shilole

Mume wa staa wa Bongo fleva na mjasiriamali Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole, Asharaf Uchebe amewachimba mkwara wanaume wowote ambao wanataka kuingilia ndoa yake na Shilole.

Uchebe amefunguka na kudai kuwa atakuwa tayari kwenda hata jela endapo atagundua kuwa kuna mwanaume anamtaka mke wake au hata atagundua kuwa anasalitiwa.

Kwenye mahojiano na Ijumaa Wikienda , Uchebe alisema kuwa anajua anapata tabu gani kuhakikisha anailinda ndoa yake hivyo ataumia sana atakapomkuta mwanaume mwingine anamrubuni mkewe na anaweza kufanya kitu ambacho hakikutarajiwa na watu wengi.

Mimi nampenda sana mke wangu najua wazi ni kiasi gani naumia kuilinda ndoa yangu isiingiliwe na kidudu mtu ila watu hawezi kuelewa hata kidogo hivyo kama nitamkuta mwanaume yeyote au nikimfumania mke wangu huyo mwanaume ama zake ama zangu”.

Shilole na Uchebe walifunga ndoa mwaka jana mwishoni.

 

Shilole Awataka Wasanii Wenzake Waolewe Ili Waache Kuzini Mwezi Huu Mtukufu

Msanii wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amewataka wasanii wenzake wa kike Kuolewa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ili waache kufanya zinaa.

Shilole ambaye alifunga ndoa na mume wake Ashraf Uchebe mwaka jana mwishoni ameonekana kifurahia ndoa hasa kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kwenye mahojiano na Ijumaa Wikienda, Shilole amekiri kuwa katika mfungo wa mwaka huu, anaona raha mno kwani ndiyo kwa mara ya kwanza umemkuta ndani ya ndoa na amekuwa akifunga na kufanya dua na mumewe tofauti na miaka mingine ambayo alikuwa hajaolewa, alikuwa akilegalega kufanya sala na kufunga.

Huu ni mfungo wa kipekee kwangu kwani ndiyo kwanza umenikuta ndani ya ndoa, kiukweli ninajisikia raha mno ambayo sikuwahi kuipata awali”.

Lakini pia Shilole aliwataka mastaa wa kike ambao hawajaolewa wajitahidi waolewe na waachane na kuzini kwa sababu dua zao ndipo zitakapopokelewa pia anawaombea ili wapate waume wema kama yeye alivyopata mume mwema anayemuongoza katika njia nzuri ya kumjua zaidi Mwenyezi Mungu.

“Sina Ujauzito Bali Nimenenepa Kwa Raha Za Mume Wangu”- Shilole

Mwanamuziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kwa jina la usanii kama Shilole amekana Tetesi za kuwa yeye ni mjamzito na kudai amenenepeana kwa sababu ya raha za ndoa.

Tetesi za Shilole kuwa mjamzito zimekuwa zikishika kasi tangu Afunge ndoa ya ghafla na mume wake Uchebe mwaka jana mwishoni.

Na taarifa hizo zinatokana na kiukweli Shilole amenenepa sana na kujiachia mwili wake kiasi ya kwamba kuwa na mwili mkubwa tofauti na alivyokuwa siku za nyuma.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Shilole alisema kuwa, amenenepa kwa ajili ya raha anazopewa na mumewe Uchebe na kuridhika na maisha yake, lakini siyo kwamba ana ujauzito.

Watu wengi wanasema hivyo, lakini mimi sina ujauzito, bali nimenenepa tu kwa raha anazonipa mume wangu,” alisema Shilole na kudai kwamba, wanaosema hivyo siyo watu wabaya kwani wanamtakia heri na mambo mazuri“.

 

Mume Wangu Hakasiriki Akiniona Nakata Viuno Hadharani- Shilole

Mwanamuziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka na kukiri haoni ubaya wa yeye kukata mauno stejini maana yupo kazini.

Suala limekuwa ishu baada ya video yake akiwa anatumbuiza stejini huku anakata kata mauno kihasara hasara stejini kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

Ndipo watu kuanza kuhoji inakuwaje mke wa mtu anafanya mambo yake hadharani lakini Shilole amewazima watu hao na kusisitiza kuwa Mume wake anajua anachofanya hivyo haoni kama kuna tatizo.

Shilole amefunguka alipohojiwa na Global Publishers kuhusu hilo na kuweka wazi kuwa anawashangaa watu wanaozungumza kuhusu hilo wakati wanajua wazi kuwa ile ndio kazi yake na mume wake Uchebe analitambua hilo hivyo hana neno juu ya hilo.

Mume wangu Uchebe (Ashraf) anajua nikiwa kazini, chochote naweza kufanya jukwaani, haoni shida maana ananipenda na kazi yangu hivyo wanaosema ninawasihi waache kwani pale nilikuwa kazini kwa hiyo lazima niwapagawishe mashabiki wangu”.

 

Harmorapa Amtolea Povu Uchebe na Kudai Ameolewa na Shilole

Rapa wa muziki wa Bongo fleva Harmorapa aliyejipatia umaarufu Kwenye mitandao ya kijamii kwa vituko vyake amerudi tena Kwenye headlines na safari hii yuko na Shilole pamoja na mumewe Uchebe.

Harmorapa ameibuka na kudai kuwa Mwanamuziki wa Bongo fleva Shilole amemuoa mumewe Uchebe. Huku akidai kuwa kitendo cha Uchebe kuacha kazi yake ya ufundi gereji na kumtegemea mke wake ni sawa na kuoelewa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmorapa amerusha dongo hili lililowaelekea Uchebe na Shilole:

Uchebe mtoto wa kiume umeachana Kupiga na spana umekimbilia Kuolewa Kwa nini badgirlshishi akuosheshe vyombo? Uchebe mtoto wa kiume rudi gereji ukapige spana la sivyo utapigwa sana vibao na shishi na kufulishwa mpaka chup*, sura yenyewe imekukunjika kama yangu utafikiri tumetoroka kwenye zui la manyani/ hiyo ndio faida ya wanaume marioo vibenteni demu wanahudumia masponsa mzigo tunakula sisi kimya kimya na chup* tunachafua sisi wahudumiaji alafu  vibenteni kama Uchebe kazi yao kutakatisha chup*”.

Shilole na Uchebe walifunga ndoa mwaka jana mwishoni, kabla hawajaoana Uchebe alikuwa fundi magari gereji lakini baada ya kufunga ndoa amekuwa akionekana kila mahali na Shilole akimsindikiza kwenye shoo zake zote hali iliyozua maneno maneno.

Shilole na Uchebe Wamefungukia Tetesi za Kuachana

Mume wa Mwanamuziki wa Bongo fleva Shilole, Uchebe amefunguka kuhusiana tetesi zilizoiandama ndoa yao mwanzoni mwa wiki hii ambapo ilisemekana kuwa wameachana.

Tetesi hizo ziliwashwa pale ambapo Uchebe aliweka UA jeusi kwenye ukurasa wake wa Instagram kuashiria penzi limeingia shubiri na baadae Shilole alilalamika kwenye redio kuwa Uchebe amempa kipigo cha mbwa mwizi.

Alipohojiwa mwandishi kutoka East Africa Tv, Shilole alikana tuhuma zote hizo na kusisitiza kuwa hajaachana na mume wake na wala hana mpango wa kufanya hivyo kwa muda wowote kuanzia sasa.

Lakini na Uchebe nae amesisitiza kuwa hajaachana na mke wake bali kuna watu ambao wanafiki hawataki kuwaona wakiwa wote na nia yao kubwa na kuwagombanisha ili waachane.

Uchebe alipoulizwa kuhusiana na lile Ua alilo liposti ambalo lilizua mambo yote hayo Uchebe alidai kuwa kuna mtu alimhack kwenye akaunti yake na kuuweka upuuzi ule.

Sio kweli sijaachana na mke wangu na wala hatufikirii kuachana, kuna watu wanafiki wanapenda kusikia tumeachana, kuhusu ile post kuna mtu alifanikiwa kuhack acount yangu na kupost vile lakini sijamuacha mke wangu, na wala hatuna ugomvi, na niwaambie tu kuwa hatuachani leo hata kiama”.

Wawili hao walifunga ndoa ya siri mwaka jana mwishoni lakini walikuja kuhalalisha kwa sherehe mapema mwaka huu.

“Nimepigwa Kama Mtoto na Uchebe Kisa Soudy Brown”- Shilole

Msanii wa Bongo fleva Shilole amefunguka na kuelezea kichapo kizito alichotembezewa na mumewe Uchebe ambapo amedai kisa na mkasa ni yeye kucheza mziki na Soudy Brown kwenye sherehe.

Siku ya jana kwenye kipindi cha XXL, Soudy Brown alifunguka kuwa alipokea taarifa kuwa Shilole alipokea kichapo kizito kutoka kwa mumewe Uchebe baada ya kurudi nyumbani usiku wa manane akitokea kwenye party Tabata.

Kupitia kwenye ‘You Heard’ Alitafutwa na kuulizwa kuhusu tetesi za kupokea kichapo hicho usiku usiku Shilole alikiri na kufunguka haya:

Tena Soudy niache kabisa wewe ndio umefanya mpaka mimi nagombana na Mume wangu eti Uchebe ana sema wewe bwana angu kweli? Umeshawahi kunitongoza wewe? Eti kisa siku ile kule Tabata tulivyokuwa tumekaa meza moja eti kakasirika, tulivyokuwa tunacheza mziki kwaiyo ina maana mimi nisicheze na mashabiki eti! MImi sitaki kuhusu kuongea mambo mengi nikaonekana mkorofi wa ajabu”.

 Lakini pia Shilole alikiri kupigwa kama mtoto na Uchebe kiasi kuwa walifunga mtaa hadi kupelekea Shilole kwenda kulala kwa marafiki zake:

Yaani Uchebe amenipiga kama mtoto mdogo lakini haina noma mimi mwanamke na dunia nzima inajua mimi mwanamke kuna mambo mimi nitakuja kusema mazito alafu ndo nitakapodai Talaka yangu”.

Baada ya sakata hilo Shilole alienda kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuweka ujumbe huu:

 

 

“Sitakubali Uchebe Aoe Mke Wa Pili”- Shilole

Msanii machachari kabisa wa Bongo fleva mwanadada Shilole amefunguka na kusema katu hatokaa akubali mume wake Uchebe aje aoe mke wa pili kwani yeye hana kasoro yoyote.

Siku chache zilizopita Mkuu wa wilaya ya Pangani, Tanga Bi. Zainab aliushangaza uma wa Watanzania na hata baadhi ya nchi za jirani kwa uamuzi wake wa kumruhusu mume wake aoe mke wa pili ili wasaidiane majukumu ya kumlea.

Baada ya sakata hilo kutrend vibaya mno kwenye mitandao ya kijamii Millard Ayo Tv ilimsaka msanii Shilole ili kumuuliza nini mtazamo wake juu ya jambo hilo kwani na yeye ni mwanamke wa kiislamu aliyeolewa na mwanaume wa kiislamu je kama ataweza kukubali Uchebe alete mke wa pili.

Kwenye Interview hiyo Shilole alifunguka haya yafuatayo:

Kwanza nikuweke wazi kabisa kuwa mimi mume wangu hawezi kuoa mke wa pili hata siku moja yaani hata kama dini inaruhusu unaoa mke wa pili ili iwaje yaani , kwanini? Yaani mimi nina  mapungufu gani mpaka ukaoe mke mwingine mtu mwingine ana mapungufu huwezi kujua lakini mimi sina mapungufu yoyote na mume wangu hawezi kuniacha na kuoa mke wa pili”.

Shilole amesisitiza wanaume wanaotaka kuoa wake wengi kibao hawaijui dini na wanaoa wake wengi kwa ulafi na tamaa lakini pia amesema endapo mume wake atataka mke mwingine basi atamuacha aoe kwa amani.

Shilole: Siwezi Kumpiga Uchebe Hayo ni Mapenzi ya Kitoto

Mwanamuziki wa Bongo fleva Shilole amefunguka na kusema kwenye ndoa yake na Uchebe hawana drama zozote hasa mambo ya kumpiga makofi hawezi kwa sababu Uchebe ni gentleman.

Shilole aliwashtua watu wengi ikiwemo familia yake baada ya kufunga ndoa ya siri iliyohudhuriwa na watu wasiopungua kumi tu nyumbani kwa Babu Tale usiku usiku huku baadhi ya ndugu zake kuonyesha wazi kutofurahishwa na jambo hilo.

Lakini tangu afunge ndoa Shilole amewashangaza wengi kwa ukimya kutawala kwani Kumekuwa na drama nyingi katika mahusiano mengi ya nyuma ya Shilole kwaiyo hali ya ukimya miezi yote hii ni hali ya kushangaza kidogo.

Lakini pia habari za Shilole kuwa mbabe na kuwachapa makofi wapenzi wake sio suala geni kwa mashabiki zake na baada ya kufunga ndoa na Uchebe wengi walikuwa wanasubiria siku Uchebe apigwe makofi ya nguvu na Shilole.

Lakini kwenye Interview aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Shilole amekiri kuwa tabia hiyo ameiacha na ilikuwa ni utoto tu fununu kuwa Uchebe ni kiburi na mkorofi zaidi yake Shilole amelieleza hapa:

Mume wangu ni like gentleman ni mwanaume ambaye ana msimamo mtu akiwa na msimamo kama hujamjua unaweza kusema ana kiburi alafu mimi nilishamjulia mume wangu anapenda nini na yeye alishajua ninapenda nini kwaiyo mambo yanaenda vizuri. Halafu suala la kumpiga makofi kwa Uchebe siwezi pale inakuwa ngumu mwenyewe unamuona yule alikuwa anapigana ana mkanda yule lakini nikimpiga nampiga makofi ya chumbani tu ya kimahaba kaniruhusu mwenyewe lakini kupigana ngumi na mume wangu haitotokea”.

Lakini pia Shilole amesisitiza kuwa tabia yake ya kupiga wanaume ilikuwa zamani ambayo ni tabia ya kitoto aliyokuwa anafanya lakini hivi sasa amekuwa hivyo hawezi kunyanyua mkono wake na kumpiga mumewe na mumewe hawezi kumpiga.

“Natamani Shilole Awe Swala Tano Kama Uchebe”- Rey Jones

Mrembo aliyewahi kuwa Meneja wa wasanii mbali mbali wa Bongo fleva kama vile Maua Sama, Msami baby pamoja na Dito huku akifanya kazi kwa karibu pamoja na wasanii wengine kama Shilole na wasanii wengine.

Rey Jones ambaye ni maarufu kama chui jike amesema anatamani sana rafiki yake Shilole awe mtu wa swala tano kama mume wake Uchebe.

Rey Jones amesema ingawa Shilole ni muislamu mzuri tu tayari lakini anatamani awe kama uchebe ambaye hakosi swala tano kwa siku.

Msanii maarufu Bongo Shilole aliuaga ukapera mwaka jana mwishoni baada ya kufunga ndoa ya siri na mume wake wa hivi sasa Uchebe ambaye ni swala tano na ameshika sana dini.

Rey Jones alimpa ushauri huo Shilole kwenye interview aliyofanya na kituo cha Dizzim Online ambpo alifunguka yafuatayo:

Uchebe ni mtu wa dini dini sana natamani na Shilole nimuone kwenye upande huo ingawa ndio yupo huko tayari lakini ana utofauti na mumewe maana Uchebe ni wale wanaitwa swala tano ile yaani kwa siku hakosi hata moja ila shishi Kama anapiga basi itakuwa moja anagusa gusa yaani mimi nataka aanze kuzipiga zote”.