Faiza Ally Amjia Juu Mke Wa Sugu Baada Ya Kupiga Picha na Mtoto Wake

Msanii wa filamu za kibongo Faiza Ally ambaye pia ni mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, amemjia juu Mke wa Sugu baada ya kupiga picha na mtoto wake.

Faiza amerudi Kwenye headlines baada ya povu lake  siku ya jana kupitia mtandao wa Instagram ambapo Mke wa Sugu aitwaye Happy, alipiga picha ndani ya ndege na mtoto wa Sugu na Faiza Sasha wakati akimtudisha Jijini Dar.

Basi baada ya Faiza kuona picha hizo aliyekuwa mbogo na kumvaa Mke wa Sugu ambapo alimtuhumu kwa kupiga picha na mtoto wake ili apate kiki na kudai hana mapenzi ya kweli kwa mwanaye.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Faiza aliandika maneno haya:

Faiza na Sugu wamekuwa Kwenye vita za mitandao ya kijamii mara kwa mara huku Faiza akimtuhumu mzazi mwenzake kwa kugoma kutoa pesa za matunzo huku akimlaumu Mke wa Sugu kama chanzo cha yote.

Faiza Ataja Sababu Ya Kuanika Ugomvi Wake na Sugu Mitandaoni

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali maarufu Kwenye mitandao ya kijamii Faiza Ally amedai sababu inayompelekea yeye kuanika ugomvi wake ni Sugu mitandaoni ni kukosa njia nyingine ya kuwasiliana naye.

Faiza na Sugu wamezaa mtoto mmoja anayeitwa Sasha na kwa muda mrefu wawili ho wamekuwa Kwenye migogoro na migogoro yao huwa Ikiwa Kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano na gazeti la Risasi Jumamosi, Faiza amedai hana njia nyingine ya kumfikishia ujumbe mzazi mwenziye huyo zaidi ya kwenye mtandao wa Instagram kwani ndio sehemu pekee ambayo atasoma na kumuelewa kwa umakini na huwa anafanya hivyo kwa sababu hakuna anayeweza kumfikishia ujumbe mzazi mwenzie huyo kwa kuwa wanamuogopa.

Mimi sinaga namba yake na ndio maana huwa naandika Instagram sababu nahisi ndio sehemu sahihi kwani nikiwatuma watu wakamfikishie ujumbe huwa wanamuogopa nikaeleza kwamba aache kutumia watu mahitaji ya mtoto, alete mwenyewe mtoto amuone”.

Siku chache zilizopita Faiza amemuanika Sugu Mtandaoni na kudai amelogwa baada ya kukataa kumpa fedha za matumizi ya mtoto wao.

Faiza Ally Adai Sugu Atakuwa Amelogwa

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali maarufu Faiza Ally amerudi tena kwenye headlines na sakata la mzazi mwenzake ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu.

Faiza amemtolea povu zito Sugu na kudai atakuwa amelogwa maana matendo anayefanya sio ya kawaida hata kidogo na anaamini hakuwa hivyo zamani wakati wako wote.

Faiza amefunguka hayo baada ya sakata lao la juzi ambapo Faiza alimtolea povu Sugu Kwenye mitandao ya kijamii na kumtaka amuheshimu baada ya Sugu kumtuma Mke wake kufanya shopping ya Faiza badala ya kumpa pesa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Faiza ameongea haya:

Kwa jinsi ninavyomjua Baba Sasha ni mtu ambaye ana akili zake lakini sijui labda kalogwa kwa sababu nilijua naye mpaka mtoto akakua kuwa na alikuwa responsible father kwa wakati huo kwa nini sasa hivi amekuwa na mwanamke mwingine amebadilika”.

Faiza aliendelea kuelekeza tuhuma za kulogwa kwa Sugu:

Mimi nadhani atakuwa amelogwa tena atakuwa amelogwa milogo mibaya ambayo yeye mwenyewe hajui kwa sababu katika hali ya kawaida huwezi kuleta matatizo Kwenye kumlea mtoto mwenyewe mmoja halafu uwezo unao kama hajalogwa atakuwa na matatizo ya akili”.