Tuzo Za SZIFF Zimerudi na Jokate Ateuliwa Kuwa Mlezi

Tuzo za Sinema Zetu zinazorushwa na kituo cha Azam Tv Kupitia chaneli Ya Sinema Zetu zimerudi tena kwa mwaka 2018.

Global Publishers wanaripoti kuwa, Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando, amesema taratibu zote za maandalizi kuelekea msimu huo mpya zimeshakamilika na kwamba zitaanza rasmi Januari Mosi, mwakani na kuhitimishwa Februari 23 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Uwasilishaji wa kazi hizo utaanza mara moja Oktoba Mosi, mwaka huu mpaka Novemba 30, mwaka huu, mchakato wote huo wa upokeaji wa kazi za wasanii utakuwa chini ya COSOTA na Bodi ya Filamu Tanzania, huku mwenyekiti wa jopo la majaji atakuwa ni profesa Martin Mhando kwani ndiye aliyekuwa pia Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar,”

Katika hatua nyingine, Tido alimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo kuwa ndiye wamempatia jukumu la kuwa mlezi wa tamasha la tuzo hizo litakalofanyika Februari 23, mwakani.

Tuzo hizo zilipofanyika mara ya mwisho zilionekana kupokelewa vizuri na wasanii na kuonekana kuondoa uhaba wa Tuzo Tanzania.