Naibu Waziri Asema,Wimbo wa Bongo Bahati Mbaya Unapoteza Dhana ya Utanzania

Kwa mara ya kwanza siku ya March 14, Baraza la Sanaa nchini pamoja na Naibu Waziri walifanya presss conference na team nzima ya XXL kutoka Clouds Media Group na kufunguka mengi juu ya wasanii na nyimbo zilizofungiwa.

Naibu Waziri na BASATA wameamua kufanya press conference hiyo ili kuzungumza na kuweka wazi mambo mengi ambayo yalikuwa yakizunguka vichwani mwa watu juu ya kufungiwa kwa baadhi ya wasanii na nnyimbo zao huku baadhi ya watu wakisema kuwa BASATA na naibu waziri wamekuwa wakifanya swala hilo kwa miemuko yao wenyewe.

Akitoa ufafanuzi juu ya sababu za kufungiwa kwa wimbo wa bongo bahati mbaya, naibu waziri anasema kuwa wimbo huo umekuwa ukitoa dhana ya utanzania kwa sababu unakuwa kama unasifia nchi za nje na kutoa uhalisia wa msanii huyo ambae anaonekana kama kujuta kuwa Tanzania.

ule wimbo umekiuka misingi ya nchi, unaondoa kabisa dhana ya kujivunia utanzania.ndio maana kuna watu wanakaa wanasema no bora kuzaliwa mbwa ulaya kuliko kuzaliwa tanzania.tumeufungia kwa kufuata sheria na taratibu kabisa.

Katika mjadala huo pia walikuwepo baadhi ya wasanii kama Vannesa Mdee ambao walikuwepo kusikiliza na kujua mambo ambalimbali kuhusu haki za wasanii .