Msanii Tekno Adaiwa Kumuiga Diamond Kwa Hili

Msanii wa muziki kutoka Nchini Nigeria anayefanya vizuri kabisa maarufu kama Tekno Miles amedaiwa kufuata nyendo Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz kwa kufungua Music Label yake.

Tekno ameingia Kwenye Listi ya wasanii wengi wa Afrika ambao wanafanya vyema kama vile Wizkid, Davido, Patoranking kwa kumiliki Music Label yake inayokwenda kwa jina la Cartel Music.

Meneja wa msanii huyo, ‘John Peace’ amethibitisha taarifa hizo katika mtandao wa burudani nchini  Nigeria kwamba Tekno ameondoka katika lebo yake ya awali  ya Triple MG na kuelekea kwenye lebo yake aliyofungua ya Cartel Records.

Msanii huyo pia amejitambulisha kuwa yeye ni mmiliki kamili wa lebo hiyo kwenye akaunti yake ya instagram kwa kuweka picha yenye jina la lebo yake ikiwa na maelezo yanayosomeka ‘CEO’.

Tekno Kuwa nje ya Muziki kwa Muda Usiojulikana

Yeye ni moja ya wasanii wakubwa na mwenye mashabiki wengi sana Duniani na hata tanzania pia amekuwa na namba kubwa ya mashabiki kiasi kwamba aliweza kuliteka soko la muziki wa tanznaia tangu ameanza kazi ya muziki.

Hii inaweza isiwe ni habari njema kwa mashabiki wa Tekno Miles kutoka Nigeria moja kati ya wasanii wenye kipaji kikubwa cha uimbaji.
Kama unakumbuka Tekno alifanya show kwenye msimu wa Tigo Fiesta 2016 na aliamsha kinoma.

Sasa mchizi huenda akaa nje ya game kwa muda usiojulikana baada ya kushauriwa na madakari ambao wanampatia matibabu kwa sasa, ambao wamemueleza kuwa anahitaji muda wa kupumzika zaidi ili aweze “ku-recover” vizuri kutokana na matatizo ya kiafya yanayomkabili.

Tekno anasumbuliwa na matatizo katika sehemu ya mrindimo wa sauti hali ambayo inamfanya kushindwa kutoa sauti vizuri, hivyo management yake kupitia kwenye ukurasa wao wa instagram imezidi kuwahimiza mashabiki wa msanii huyo kumuweka kwenye maombi ya kila siku ili Mungu aweze kumpatia wepesi na kurudi tena kwenye kazi zake kama kawaida