Times Fm Yaomba Radhi Baada Ya Interview Ya Diamond

Kituo cha redio cha Times Fm imeomba radhi baada ya Interview yao waliofanya na supastaa wa Bongo fleva Diamond Platnumz wiki chache zilizopita.

Baada ya Diamond kuachia albamu yake ya ‘A boy From Tandale’ alienda katika kituo cha Times Fm katika kipindi cha The Playlist kwa ajili ya kufanya mapitio ya Albamu yake mpya.

Kwenye Interview hiyo Diamond aliwatolea povu zito BASATA ambayo ilikuwa imefungia nyimbo zake mbili kwa wakati huo ambazo hakuweza kuzifanyia marejeo.

Siku ya jana Diamond alimaliza bifu lake na BASATA na hata Waziri Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri Juliana Shonza na kufungulia nyimbo zake hizo mbili

Barua ya kuomba Radhi kutoka  Times Fm:

Baada ya Kumjohi Diamond, TCRA Kuichunguza Times Fm

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA  imesema kuwa kamati yake ya maudhui inafatilia kipindi alichofanya Diamond Platinumz katika radio ya Times Fm iliyofanyika siku za hivi karibuni huku kipindi hicho kikiongozwa na Lilommy.

Mkuu wa idara ya mamlaka hiyo amesema kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona mahojiano hayo na pia kituo icho kipo katika vituo wanavyovisismamia.

Diamond alifanya mahojiano na kituo icho na kusema mambo mengi ambayo hayakuwahi kujulikana katika jamii, lakini kubwa zaidi ni kufunguka hasira zake baada ya kufungiwa kwake na wasanii wenzake kupigwa kwa baadhi ya nyimbo zao katika vituo mbalimbali .

Kwa namna nyingine inaweza kusemekana kuwa mahojiano hayo ndio yaliyozua migogoro yote inayoendelea sasa kati ya Diamond na mamlaka ya inayohusiaka na mambo ya sanaa.