Wema Kaja na Hili Jipya Kuchombeza Kuwa Karudisha Majeshi Kwa Diamond

Diamond Platnumz ameachana na Zari mwezi uliopita na tangu hapo Kumekuwa na fununu za wanawake kadhaa kuchukua nafasi yake lakini Wema amerudi kwenye nafasi ya kwanza.

Kumekuwa na tetesi nyingi za kuwa Diamond amerudiana na aliyekuwa mpenzi wake miaka michache iliyopita, Wema Sepetu.

Siku ya leo ni kama Wema amezidi Kutia petroleum kwenye tetesi za yeye kurudisha penzi kwa Diamond kwani ndo zinazidi kuwaka moto.

Siku ya jana Wema alitajwa na watu kadhaa kutoka WCB kuwa kama African beauty na moja ya watu hao ni Harmonize ambaye alimtag Wema kama African beauty wake na Wema alijibu Mapigo kwa posti  hii aliyotupia kwenye ukurasa wake wa Instagram:

Lakini pia Wema hakuishia hapo kama utakumbuka Zari alivyompiga Diamond kibuti siku ya Wapendanao alitumia Ua la rangi nyeusi kuashiria penzi lililokufa lakini leo Wema kaposti Ua la rangi nyekundu kuashiria penzi lilohai na tamu.

Posti hiyo inazidi kuibua tetesi kuwa inawezekana Wema anamrusha roho adui yake namba moja Zari baada ya kurudiana na Diamond.