Ben Pol Kufanya Remix na Tanzania All Stars

 

    

                                                     Willy Paul akiwa studio na Ben Pol

Msanii anaefanya vizuri katika kazi za muziki kutoka kenya willy paul hivi karibuni alikuwa tanzania na alibahatika kufanya mahojiano katika vituo mbalimbali vya habari na katika moja ya mahojiano yake willy aliweka wazi kuwa ameshirikishwa wimbo na ben pol , wimbo ambao ni remix ya moja ya nyimbo zake lakini jambo la kufurahisha zaidi ni kwamba ben pol ameamua kuwaweka mastaa kibao katika wimbo huo.

Willy Paul alisema kuwa katika wimbo huo ben pol alimwambia kuwa nataka kufanya kazi na wasanii wakubwa wa bongo lakini aliamua kumpa nafasi na yeye hivyo kwake ni jambo la kumshukuru Mungu.

Juzi nilikuwa na Ben Pol na amenishirikisha katika wimbo wake fulani na ameniambiani all stars,anafanya remix ya one of hus songs na pale nimemuona kuna vannesa mdee. joh makini, Nandy , joh makini na mimi pia. Siwajui wote lakini kuna Barnabas na Ben pol mwenyewe.

Akizungumzia jinsi alivyofurahi kujiona katika wasanii watakaofanya kazi na wasanii wengine wakubwa wa bongo Willy Paul anasema “nashukuru mwenyezi mungu kwa kila kitu ananipatia kiwe kikubwa au nikidogo ninashukuru kwa sababu ananipatia baada ya kuona kuwa nimekuwa nikimtumikia kwa muda mrefu.”

Willy Paul anasema kuwa yeye ni mwanamuziki ambae anaimba nyimbo za injili lakini pia za mapezni lakini hajwahi kuimba nyimbo zinazoonyesha uchafu wowote kwa sababu yeye anamtumikia mungu na nyimbo anazoimba anataka myu aweze kusikiliza na mpezni wake au mzazi wake , kwaio yeye ni muimbaji mzuri wa nyimbo za mapenzi.