Meneja wa Yamoto Band hakana kuwa Aslay anapendelewa

Chambuso ambaye ni meneja wa bendi la Yamoto Band amefunguka kwa mara ya kwanza kukana kuwa Aslay anapendelewa zaidi kushinda mtu yeyote kwenye bbendi hiyo.
Akizungumza kwenye kipindi cha Daladala Beat alisema kuwa wasanii wa bendi wanapewa nafasi zinazotoshana na hakuna Yule ambaye ako juu ya mwingine. Maneno haya yalikuja baada wengi kufikiria kuwa Aslay anasaidiwa na management ya Yamoto kufanya kazi zake solo na ndio mana anaonekana akifanya vizuri.

“Hapana, Aslay anafanya kazi pekee yake na management yake, pia Maromboso atakuwa anafanya na management yake na watakuwa na vikao vyao na kushauriana jinsi ya kutoa nyimbo na hao wengine.”

Aliendelea kwa kutoa mfano mwingine wa Beka ambaye pia anafanya project zake solo. Chambuso alisema,

“Unaona kama wimbo wa Beka, Mkubwa na Wanawe hatujahusika. Ni yeye na management yake ndio wametoa, kwa hiyo sidhani kama Aslay anapendelewa kwa sababu kila mmoja ana management. Hakuna mtu anayependelewa, sisi kama uongozi wa Yamoto tunafanya vitu kwa usahihi, kama Aslay anastahili kulipwa laki atalipwa, na kila mtu alikuwa anaandika verse mwenywe hakuna mtu aliyekuwa anaandikiwa verse, kwa hiyo kila mtu alikuwa anapewa nafasi kufanya kile alichokuwa anafikiria,”