Bifu la Amber Lulu na Young Dee Lapamba Moto

Msanii wa Bongo fleva na hitmaker wa Bongo Bahati Mbaya Young Dee ameingia Kwenye bifu zito na aliyekuwa mpenzi wake na msanii mwenzake Lulu Eugenn maarufu kama Amber Lulu.

Bifu la Amber Lulu na Young Dee lilianza Siku za nyuma baada ya Amber kumtuhumu Young Dee kwa kumpa kipigo studio baada ya kumuona akiwa na mwanaume mwingine.

Amber Lulu alimtolea povu zito Young Dee baada ya picha zake za Harusi kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii ambapo Amber rapa huyo hawezi kuoa kwa sababu hicho si kitendo rahisi na ukiangalia yeye mwenyewe sasa hivi anatamani kuolewa, hivyo kumtaka afanye muziki bila kutengeneza kiki kama anaweza.

Global Publishers lilimtafuta Young Dee Baada ya povu Amber ambapo Meneja alifunguka:

Young Dee hawezi akabishana na mtoto wa kike halafu hata hivyo huyo Amber Lulu hawezi akafanya muziki mzuri bila kufanya kiki na tena ukiangalia kiki zake nyingi ni lazima amtaje Young Dee, kwa sababu anajua kuwa brand kubwa hivyo anaona akimtumia lazima atoboe”.

Amber Lulu naye alifunguka tena kuhusu Young Dee ambapo aliendelea kumtolea shombo baada ya kusema anahitaji kuolewa kwani hawezi kuoa:

Niliongea vile kwa sababu najua Young Dee hawezi akatoa wimbo bila kufanya kiki, anadanganya watu kuoa wakati yeye mwenyewe anahitaji mtu wa kumuoa, halafu ukiangalia kiki ni kubwa kuliko wimbo anaotaka kuutoa yani kiufupi siku hizi muziki wake ushakufa labda ajipange upya“.

 

 

Alichojibu Young Dee Kuhusu Kumpiga Amber Lulu.

Msanii wa bongo fleva Young Dee amefunguka na kujibu tuhuma za kuwa aliwahi kumpiga maber lulu wakiwa studio huku sababu kubwa ikiwa ni kwamba Young Dee bado anampenda amber lulu na amekuwa akimuonea wivu kla anapomkuta na mwanaume mwingine hata kama hawana mahusiano.

Amber Lulu ambae alithibitisha hilo alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wa habari na kusema kuwa ni kweli waligombana na Young Dee kutokana nawivu wake wa kumkuta akiwa karibu na meneja wake anasema kuwa hata yeye hana mpango wa kutoka tena na young dee kwa sababu alishapi huko siku nyingi.

Alipoulizwa kuhusu swala hilo, young dee alisema” mimi na Amber Lulu sio washkaji kwaio hata sitaki kuzingumzia taarifa kama hiyo , mi siwezi kuzungmza kwenye intrview kubwa kama hii nikamzungmzia  nikazungumzia watu ambao  hawanihusu