TID: Wasanii wananyanyaswa na wadau wa muziki

TID amelalamika kuhusu rushwa ambayo wasanii wanalazimishwa kutua na wadau wa muziki. Staa huyo anadai wasanii wananyonywa na wadau ambao wameweka pesa mbele.

TID anasema kuwa kuna baadhi ya wadau ambao wanaomba rushwa kutoka kwa wamamuziki ile ngoma zao ziweze kupenya kwenye masikio ya mashabiki.

download latest music    

Hit maker huyo wa kitambo anasema kitendo hicho kimewalazimisha wasanii wengi kutenga bajeti ya kufanya matangazo ya kutosha ili kazi ziweze kusikika mitaani na sehemu mbalimbali.

“Nakerwa sana na watu ambao hawajui jinsi gani sisi tunasumbuka. Unalipa studio, video na mambo kibao kwa ajili ya kufanikisha kazi, cha ajabu DJ anaweza akataka kupiga lakini mtangazaji anakwambia acha mpaka atoe kitu huu ni uuaji wa vipaji na ninapigana nao sana. Sasa wameshatujengea kwenye mindset kuwa ukiandaa ngoma andaa na pesa ya kutulipa ili kazi itembee” TID alisema akiwa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere