Vanessa Mdee aonya msanii mkongwe anayemsemea maneno machafu

Vanessa Mdee anadai kuwa kuna msanii mkongwe anamchafulia jina lake kwa kumtaja katika kashfa kadha zisizoeleweka.

Vee Money hata hivyo hakuweka wazi jina lake mwanamuziki huyo mkongwe ambaye anadai  anamsemea maneno machafu.

download latest music    

“Inasikitisha kwamba mtu ninayemheshimu na kumtambua kwenye hii sanaa kila kukicha jina langu mdomoni mwake kwa kashfa zisizoeleweka,” Vanessa Mdee aliandika kwenya mtandao wa Twitter.

Mrembo huyo alitoa onyo kwa kusema kwamba hawezi jibishana na msanii huyo mkongwe kwasababu anampa heshima zake.

“Siwezi kujibishana na wewe itakuwa utovu wa nidhamu baba.,” Vanessa aliongezea.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere