Vanessa Mdee: Collabo za kimataifa zinafurisha akaunti yangu ya benki

Vanessa Mdee anavuna faida ya kufanya collabo na wasanii kutoka nchi zingine. Mwimbaji huyo amekiri kuwa collabo za kimataifa zinamletea pesa nyingi sana.

Akiongea na Bongo5, Mdee alisema kuwa collabo zake na wasanii kutoka Malawi na Nigeria zimemfungulia mlango kufanya shows katika nchi hizo.

download latest music    

Mdee anasema yeye hupata pesa nyingi kutoka kwa shows anazofanya nje ya nchi.

“Yeah collabo hizi definitely zinaamisha more money in the bank, sababu kama mimi Malawi nilikuwa sijawahi kwenda kufanya show sasa hivi nimeshakaribishwa kwenye matamasha mbalimbali so more money in the bank. Pamoja na Nigeria, kesho kutwa naenda kufanya show Gidi Fest, ni tamasha kubwa, nilishawahi kufanya lakini sasa hivi nina content nyingi zaidi ambazo zina wasanii wa Kinaijeria so nyimbo zinakuwa zinafahamika na mashabiki wengi zaidi huko so definitely more money in the bank because to me every fan is a blessing na wanaendeleza muziki wangu wanaufikisha pande ambazo hata mimi sijawahi kufika,” Vanessa Mdee alisema.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere