Vitu Mwanamke Anapaswa Kuepuka Kufanya Kwa Mwanaume

Katika maisha ya mapenzi watu wanapaswa kulewana na kusikiliza , hii ndio njia sahihi na rahisi zaidi ya kukaa pamoja kwa muda mrefu lakini pia itasaidia wawili wanaopenda kudumu katika mahusiano yao.Ikitokea mwanamke akamsikiliza vizuri mwanaume na mwanaume akamsikiliza vizuri mwanamke basi mapenzi ya watu hawa yanaweza kuwa mfano kwa watu wengine.

moja ya vitu watu wemgi tunakosea katika mapenzi ni kujipa thamani na kujijali zaidi kuliko wenzi wetu,jitahidi kumthamini mwenzio, na huo ndo upendo mkubwa ambao hata mwenyezi Mungu alituagiza.

download latest music    

Wasichana wengi wamekuwa wakikosea baadhi ya vitu , inawezekana kwa kujua au kutokuja kabisa anajikuta mahusiano  yake yanakatika ghafla.Endapo utajitahidi kwa msichana kuepuka yafuatayo , itakusaidia kuboresha mahusiano yako.

1.kuzungumza sana

Wanaume wengi hawapendi wanawake wanaoongea sana au wako mapepe sana.Inawezekana kuwa ni tabia yako kupiga soga unapokuwa na watu uliowazoea hasa mashosti zako, lakini jitahidi kubadilika na kuwa na spidi  unapokuwa na mpenzi wako.Usijifanye kuwa unajua kila kitu,jitahidi kuongea maneno ya kufariji, kutia moyo, au kumfanya apumzike na kuondoa mawazo aliyonayo.Haimaamisie kwamba uigize kuwa mkimya maana hatakapogundua pia itakuwa shida ila jitahidi kuongea maneno kidogo na yeye maana, mwanamke anashauri kuwa na uchaguzi wa maneno kwa mwanaume.

2.kumzingua mnapokuwa faragha.

Wapo wanawake ambao muda wote wao wanakuwa na udhuru, anakuwa anasema anampenda mwanaume aliyenae kwenye mahusiano lakini kila siku anampiga tarehe, je unategemea starehe mwanaume wako aliyokuwa akiitegemea kwako ataipata kwa nani, mwisho wake ataanza kuchepuka na utalalamika pia.Mwanaume ana haki juu ya mwili wa mwanamke, na mwanamke vilevile. Sio kila siku wewe umechoka au unaumwa.

3.kutokumheshimu mwanaume.

Ni kitu kisichopingika kuwa wanaume wote wamelelewa katika misingi ya kuwa kichwa cha familia,hivyo wanapoona wanahesimiwa na watu wao wa karibu wanakuwa na upendo zaid.Kwani kuna shida gani ukimpenda na kumheshimu mwanaume wako.Acha kumuogopa maana huko kutawafanya mkose kuwa na uhuru kwa kila mmoja wenu, mpe heshima yake mwanaume mbele ya watu na hata mnapokuwa wawili , heshima ni kitu ambacho kila mwanaume anakitamani kutoka kwa mpenzi wake.

4.Kumbadilisha mwanaume kwa haraka

Kila mtu amekulia katika maisha yake na nyie kama wapenzi mmekutana tu ukubwani,kuna vitabia na mazoea mabaya kila mtu alikuwa nayo kabla hamjakutana, mwanamke usikurupuke kuanza kumwambia mwanaume sitaki hiki au sitaki tabia hii au sitaki unavyofanya hivi,kila kitu uanza polepole , cha kufanya ni kuzisoma na kuzielewa tabia zake na ikibidi kujua kwanini anapenda kufanya kitu icho.Hata kama kina ubaya kiasi gani, haipaswi kumlazimisha kwa gafla kumbadilisha, kuna baadhi ya wadada ufikia hatua ya kusema kama hautoacha kitu flani basi mimi na wewe basi, hapana mapenzi hayako hivi, inabidi kuelewana na kusaidiana kwa kila kitu.Lakini pia kumbuka unapomkataza tabia moja au kitu kimoja absi jiathidi kumatafutua njia nzuri ya kuondikana na kile usichokihitaji.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.