“Wanamkufuru Mungu kwa sababu Mungu ndiye anayepanga na kupangua,” Harmorapa ambia watu wanaomuongela vibaya

Image: Harmorapa

Staa na rapa wa Tanzania, Harmorapa hivi majuzi aliweza kufunguka kuhusu watu ambao wanamtusi na kumuongelea vibaya tangu awe maarufu.

Rapper huyo ambaye amekuwa akifanya vizuri Tanzania na Afrika Mashariki kupitia nyimbo zake hivi sasa ndiye anayepata kiki kubwa Bongo na anavyoonekana, Harmorapa atakuwa na umaarufu kama wa Diamond Platnumz iwapo ataendelea kurelease projects ambazo watu watapenda.

download latest music    

Hata hivyo, akizungumza na Bongo 5 rapa huyu alisema kuwa habebwi na kiki na kuwa kazi yake ndiyo inafanya awemaarufu kwa hivyo wanomchukia wanafanya kazi bure na kuwa ataendelea kuachilia nyimbo zake kama kawaida.

“Watu ambao wanahisi Harmorapa hatodumu kwenye game kwanza wanakosea halafu pia naweza nikasema kwamba wanamkufuru Mungu kwa sababu Mungu ndiye anayepanga na kupangua,”

Aliendelea kwa kusema kuwa…

“Kama mimi binafsi nimejipanga sana vya kutosha. Unajua kwamba maneno yao mimi hayanivinjii chochote ni ile sawa na kumpiga chura teke na kumwongezea mwendo. Wanavyoniongea mimi ndo wananipa power na wananipa maujuzi na wananipa kuweza. Ni wao wananiweza mimi kuweza na kukaza ilmradi niweze kufanya kazi nzuri.”

Harmorapa  pia amehaidi mashabiki wake projects kubwa ambazo ataachilia mwaka huu.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua